VIUNO alivyokatika staa maarufu wa
filamu, Jacqueline Wolper viliwachengua ile mbaya watu waliohudhuria
harusi ya wasanii maarufu wa Bongo Movies, Jimmy Mafufu na Idrissa
Makupa ‘Kupa’.
Tukio hilo lilitokea hivi karibuni
katika Ukumbi wa Urafiki uliopo Ubungo, jijini Dar baada ya wasanii
kwenda mbele ya ukumbi kwa zamu na kuonyesha uhodari wa kuyarudi mangoma
ambapo ilipofika zamu ya Wolper, alionekana kuwazidi wenzake kwa utundu
wa kucheza.
Baada ya kuonesha vitu adimu ambavyo
havikuoneshwa na staa yeyote kati ya waliomtangulia, wageni waalikwa
walishangilia na kupiga makofi hadi aliporejea sehemu aliyokaa awali.
source: globalpublishers.info
No comments:
Post a Comment