Hali si shwari KAWE Jana jioni ..... Dereva wa Bajaj apigwa hadi kufa na kutupwa mtoni.
Kumekuwa na
hali vurugu kubwa katika kituo cha Polisi KAWE jioni ya jana baada ya
Wananchi kuvamia kituo hicho na kuzua balaa kubwa kwa kurusha
mawe,kufanya fujo huku wakipiga kelele kiasi cha kuwafanya Polisi
watumie risasi kwa ajili ya kutuliza amani .
Inasemekana chanzo cha
ghasia hizo ni kifo cha dereva mmoja wa Bajaj huko Kawe Ukwamani
aliyesadikiwa kupigwa hadi kufa na Askari wa jeshi la kujenga Taifa na
baadae kutumbukizwa katika mto jana mchana (kama inavyoonekana pichani).
Hadi sasa chanzo kizima cha kipigo hicho hakijajulikana ila fununu
zilizopatikana zilieleza kuwa ni upotevu wa simu ya mmoja ya Wanajeshi
hao .
No comments:
Post a Comment