Wakati Tanzania imetajwa kuwa nchi ya pili kwa umaskini kwenye
ukanda wa Afrika Mashariki, wabunge wameishukia Serikali kwa kutenga
fedha kidogo kwenye Bajeti ya Kilimo.
Utafiti uliofanywa na Benki ya Dunia na
Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), unaonyesha kuwa Burundi ndiyo nchi
inayoongoza kwa kuwa na watu wengi maskini ikifuatiwa na Tanzania kwenye
eneo hilo.
Burundi inaongoza kwa kuwa na asilimia 81.32, Tanzania ikifuatia na asilimia 67.87, Rwanda asilimia 63.17, Kenya asilimia 43.37 na Uganda 38.01. Utafiti huo ulijikita zaidi katika kuangalia idadi ya watu wanaoishi kwa Dola 1.25 kwa siku.
Burundi inaongoza kwa kuwa na asilimia 81.32, Tanzania ikifuatia na asilimia 67.87, Rwanda asilimia 63.17, Kenya asilimia 43.37 na Uganda 38.01. Utafiti huo ulijikita zaidi katika kuangalia idadi ya watu wanaoishi kwa Dola 1.25 kwa siku.
Jana, baadhi ya wabunge wakiwamo wa CCM, walikataa kuunga mkono Bajeti ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika wakisema haiwezi kuinua maisha ya wakulima, ambao ni asilimia 70 ya Watanzania.
Mbunge wa Kahama (CCM), James Lembeli alikuwa wa kwanza kuchangia bajeti hiyo na kusema baada ya kufuatilia kwa makini maelezo ya waziri, hakuna taarifa njema kwa wapigakura wake hivyo hawezi kuunga mkono hoja hiyo.
Alisema kwenye hotuba ya waziri hakuna sehemu ambayo imekuja na suluhisho la matatizo ya wakulima nchini na akisema ni ukurasa wa 50 tu ambao unataja rasimu ya kuanzisha mfuko wa bei ya mazao.
Lembeli alisema hotuba hiyo imewaacha wakulima kwenye mazingira magumu ya kukata tamaa na hasa wale wa pamba na tumbaku kwenye jimbo lake...
“Akilima ekari moja ya pamba kipato chake
kwa mwaka hakizidi Sh200,000 sasa leo Serikali inakuja inasema imekuja
na rasimu, imekamilisha… ah, siungi mkono hoja.” Alitaka kujua jinsi
Serikali ilivyojiandaa kupambana na bei ya pamba iwapo itashuka.
Alisema jimboni mwake kuna wakulima wazuri wa tumbaku wanaoliingizia taifa Sh15 bilioni kwa mwaka, lakini... “Wakulima wa tumbaku wanabambikiwa madeni, matokeo yake mwisho wa mwaka hawalipwi, nimepiga kelele, nimemwomba waziri atembelee sijui ameweka nini masikioni mwake, hasikii.”
Alisema matokeo yake, viongozi wa Serikali hasa ofisa ushirika wa wilaya, ambaye alisema hayupo kwa masilahi ya wakulima ndiye anayechonga michongo ya kuwaibia wakulima.
Lembeli alisema kuna wakulima ambao waliuza mazao tangu mwaka jana na hadi sasa hawajalipwa akisema dhuluma inajionyesha zaidi kwenye uuzaji... “Hivi ni kwa nini tumbaku inanunuliwa kwa Dola, pembejeo inakopeshwa kwa Dola lakini mkulima analipwa kwa shilingi, hii ni nini, ni wizi mtupu.”
Akichangia Bajeti hiyo, Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige (CCM) alisema: “Mabonde mazuri yapo, lakini Waziri wa Kilimo (Christopher Chiza) ni rafiki yangu tumekuwa tukizungumza naye mara kwa mara, lakini naamini hapa tulikofika wananchi wangu wa Shinyanga ni marafiki zangu zaidi, hakuna hata skimu moja ya umwagiliaji.”
Alisema kuna mabonde ya Msalala na Solwa, yanayotosheleza kuzalisha mazao mengi kuliko Mbarali (Mbeya), lakini kinachofanyika ni kutosikilizwa kwa wananchi wa Shinyanga kwenye matatizo yao.
Maige ambaye mwaka jana alikuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, alisema kilimo cha pamba kinaendesha maisha ya zaidi ya watu milioni 14, lakini wanaendelea kupata hasara kwa kuwa hakuna mfuko wa kuwalinda pindi bei inapoporomoka.
CHANZO MWANANCHI.
No comments:
Post a Comment