MKANDARASI wa jengo la ghorofa 16 lililoporomoka Ijumaa iliyopita na
kuua watu kadhaa kwenye Mtaa wa Indira Gandhi jijini Dar es Salaam, Raza
Hussein Raza, na wenzake 10 jana wamepandishwa kizimbani kwenye Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini.
Washitakiwa hao wamesomewa
mashitaka 24 ya kuua bila kukusudia. Katika kesi hiyo mawakili wa upande
wa utetezi waliwapigania wateja wao kupata dhamana lakini upande wa
mashitaka ulipinga ombi hilo na kuzua mjadala mzito ulioshindwa
kupatikana suluhu.
Washitakiwa wamerudishwa rumande mpaka kesho kesi hiyo itakapotajwa tena mahakamani hapo.
(PICHA: RICHARD BUKOS NA ISSA MNALLY / GPL)
Mkandarasi Raza Hassan Raza akiinama tayari kusujudu baada ya kufikishwa mahakamani.
Akiwa kaifikia ardhi kwa ajili ya kusujudu.
Askari akiwaongoza watuhumiwa kuelekea kizimbani.
Mkandarasi Raza Hassan Raza akiinama tayari kusujudu baada ya kufikishwa mahakamani.






No comments:
Post a Comment