EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, April 4, 2013

Watuhumiwa wa ujambazi 25 wakamatwa Kinondoni.

JESHI la Polisi Mkoa wa Kinondoni, limefanikiwa kuwakamata watu 25 wanaotuhumiwa kwa kujihusisha na ujambazi wa kutumia silaha, pikipiki na magari katika kufanikisha uhalifu wao.
Akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alisema watuhumiwa hao walikamatwa katika kipindi hiki cha sikukuu.

Alisema watuhumiwa hao ni wale wanaofanya uhalifu kwa kuvunja madirisha na kisha kuloa simu na mali nyingine zinazobebeka kwa kutumia ndoano iliyofungwa kipande cha wavu kwa kutumia kitambaa cha chandarua kilichofungwa misili ya goli la kwenye mchezo wa mpira wa kikapu.

“Mbinu hiyo ya uhalifu imepewa jina la Jordan, ambalo ni la mchezaji maarufu wa mchezo wa mpira wa kikapu aitwaye Michael Jordan.

“Wahalifu hao pia hutumia mbinu ya kufanya ujambazi kwa kukata makufuli na makomeo ya milango kwa kutumia mikasi maalumu, ambayo huweza kukata kitu chochote na kufanikisha kuingia mahala ambapo wamepadhamiria kufanya uhalifu.

Alisema miongoni mwa watuhumiwa waliokamatwa ni wale waliowahi kufanya matukio mbalimbali ya uhalifu katika maeneo ya Kinondoni na Jiji la Dar es Salaam.
Matukio hayo kwa mujibu wa Kenyella, ni pamoja na wale wanaojihusisha na wizi wa magari ambapo Machi 27 mwaka huu huko eneo la Kinondoni Mtambani, majambazi watatu walipora gari No T 331 BPK aina ya Toyota Rav4 na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao ambao walikiri kupora gari hiyo.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Ayoubu Mohamed (20), Mkude Said (28) na Deogratius John(23) ambao wote ni wakazi wa Dar es Salaam.

Alisema upepelezi juu ya watuhumiwa hao unaendelea ili waweze kufikishwa mahakamani.

Kwa mujibu wa Kenyella, Polisi pia inawashikilia wezi wa bajaj zilizoibiwa katika eneo la Oysterbay, watuhumiwa wengine wawili wanaojihusisha na ukwapuaji wa mikoba kwa kutumia pikipiki.

Katika msako wao huo, pia walifanikiwa kukamata silaha mbalimbali, ikiwemo Bunduki aina ya shortgun iliyokamatwa eneo la Kigogo round about na bastola aina ya Glock 19 yenye namba LZB 642 na T CAR 98189 ikiwa na risasi 12 katika magazine iliyokamatwa Mabibo.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate