Watu wanne wamenusurika kufariki dunia baada ya udongo wenye
mawe kuwafukia chini katika shimo zaidi ya saa 12 walipokuwa wakichimba
dhahabu katika Kijiji cha Patamela wilayani Chunya.
Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Deodatus Kinawiro alithibitisha k wa njia ya simu jana juu ya tukio hilo na kwamba lilitokea Ijumaa iliyopita, ambapo uokoaji ulifanywa na Kampuni ya Shanta Gold Mining inayochimba dhahabu kilometa 10 kutoka eneo la tukio.
Kinawiro aliwataja walionusurika kuwa ni Antony Rwegasira(28), Pascal Claud(33) , John Gideon(47) na Noni Kwandu (40) wote wakazi wa wilayani humo.
“Ni kweli lango la kuingia shimoni
liliporomoka, lakini gogo lilinasa kwenye mwamba na kusababisha mawe
makubwa yabaki eneo hilo’’, alisema
Aliishukuru Kampuni ya Shanta kwa msaada iliyotoa kuokoa maisha ya watu hao na kwamba bila ya vifaa vya kampuni hiyo wangekuwa marehemu.
Aliishukuru Kampuni ya Shanta kwa msaada iliyotoa kuokoa maisha ya watu hao na kwamba bila ya vifaa vya kampuni hiyo wangekuwa marehemu.
Naye Msemaji wa Kampuni ya Shanta Gold Mine, Roman Urasa alisema kazi ya uokoaji ilifanikiwa baada ya Mwenyekiti wa Kijiji cha Saza, Philip Mwakitalima kumpigia simu saa tano usiku Meneja Mkuu wa Kampuni ya Shanta Mining Chunya, Braam Jankowitz akiomba msaada wa kuwaokoa watu hao.
“Jankowitz kwa haraka alikubali kusaidia na kuipanga timu yake ya uokoaji kwa ajili ya kwenda kwenye eneo la tukio ambalo lipo umbali wa takriban kilomita 10 na walifanya kazi pale kuanzia saa sita usiku hadi saa mbili asubuhi alipookolewa mtu wa kwanza.
No comments:
Post a Comment