CHELSEA imefanikiwa kutinga fainali ya
Europa League baada ya kuifunga mabao 3-1 FC Basle ya Usiwsi usiku huu
kwenye Uwanja wa Stamford Bridge.
Mabao ya Chelsea katika mchezo huo
yalifungwa na Fernando Torres dakika ya 50, Victor Moses dakika ya 52 na
David Luiz dakika ya 59, wakati la kufutia machozi la Basle lilifungwa
na Salah dakika ya 45,
Chelsea imetinga fainali kwa ushindi wa
jumla wa 5-2, baada ya awali kushinda ugenini 2-1 na sasa itamenyana na
Benfica ya Ureno katika fainali, ambayo usiku huu imeifunga Fenerbahce
mabao 3-1 hivyo kufuzu kwa jumla ya ushindi wa mabao 3-2.
Katika mchezo wa leo, kikosi cha Chelsea kilikuwa;Cech, Azpilicueta, Ivanovic, Cahill, Bertrand, Lampard, Luiz/Ake dk81, Ramires/Oscar dk66, Hazard/Mata dk75, Moses, Torres.
Basle:
Sommer, Steinhofer, Schar, Sauro, Voser, El-Nenny, Frei/Diaz dk62, Die,
Salah, Streller/Zoua dk75, Stocker/David Degen dk62.
Kitu hicho: David Luiz akifunga kwa shuti la mbali
Hakuna kukosea: Victor Moses akifunga
Victor Moses
Mtelezo wa bao: Fernando Torres akifunga bao lake la tano katika mechi nane na la 10 katika Europa League msimu huu
No comments:
Post a Comment