DAKTARI
wa meno wa Hospitali ya Wilaya ya Morogoro, Alnord Limo anayekadiriwa
kuwa na umri wa miaka 40, amekutwa amefariki dunia kwenye chumba cha
gesti huku habari zikidai alijinyonga kwa shuka.
Mkasa
huo ulimfika daktari huyo Jumatano iliyopita kwenye nyumba ya kulala
wageni ya Camel iliyopo Kihonda, kandokando ya barabara kuu ya Morogoro
kwenda Dodoma.
Mhudumu wa gesti hiyo ambaye aliomba hifadhi ya
jina, kwa kuwa si msemaji mkuu wa kazini kwake, alidai siku ya tukio
marehemu alifika kwenye gesti hiyo na kukodi chumba namba 2 ambapo
walimchukulia kama mteja wa kawaida.
”Alikuja na kuomba chumba,
tukampa namba mbili. Aliingia akiwa peke yake, lakini baada ya muda
alitoka na kuja mapokezi, sijui alikuwa na shida gani, halafu akarudi
tena ndani,” alisema mhudumu huyo.
Aliongeza kuwa asubuhi walipoona
hatoki na muda wa kuondoka ulifika, ndipo walipoingiwa na wasiwasi na
kwenda kufungua ambapo walimkuta amekufa.
Habari za ndani zaidi zilidai kwamba, daktari huyo alifunga ndoa miezi mitatu iliyopita na kwamba siku ya tukio mkewe alikuwa safarini.
Habari za ndani zaidi zilidai kwamba, daktari huyo alifunga ndoa miezi mitatu iliyopita na kwamba siku ya tukio mkewe alikuwa safarini.
Inadaiwa siku moja
kabla ya tukio hilo alikusanya nguo zake na simu ya mkononi na kupeleka
kwenye kambi ya kulea watoto yatima ya Mgolole iliyopo mjini hapa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile alipohojiwa na mwandishi wetu alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa marehemu hakuacha ujumbe wowote.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile alipohojiwa na mwandishi wetu alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa marehemu hakuacha ujumbe wowote.
No comments:
Post a Comment