Mwanza.
Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Mwanza(TPA),Edwin Kasyupa ameitaka Serikali kutambua umuhimu wa maadhimisho ya kuzama kwa meli ya Mv Bukoba huku mwanamitindo Flavian Matata akitoa msaada wa maboya 500.
Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Mwanza(TPA),Edwin Kasyupa ameitaka Serikali kutambua umuhimu wa maadhimisho ya kuzama kwa meli ya Mv Bukoba huku mwanamitindo Flavian Matata akitoa msaada wa maboya 500.
Akizungumza katika kumbukumbu ya ajali ya meli hiyo ambayo ilitokea miaka 17 iliyopita,Kasyupa alisema kuwa Serikali haijatoa mkazo katika kumbukumbu ya ajali ya Mv Bukoba hivyo imeonekana kuwa kama siku ya walengwa waliopoteza ndugu na jamaa zao badala ya kuwa ya kitaifa.
Meli ya Mv Bukoba ilizama Mei 21,1996 na kukadiriwa kuua watu zaidi ya watu 800 ingawa wakati inaondoka inadaiwa meli hiyo ilikuwa na watu zaidi ya 1,200.
“Msiba huu ni wa Taifa, lakini kwa sasa unaonekana kama ni wa walengwa pekee wakati watu wote tulipata mshtuko na kufiwa, haitoshi kuwaachia walengwa pekee yao hivyo Serikali inapaswa kulitambua hili na ikiwezekana ifanye kuwa siku maalumu itakayo adhimishwa kitaifa,”alisema Kasyupa.
Kwa upande wake Meneja wa Masoko wa Huduma ya Meli(MSC), Nahodha Obedi Nkongoki alisema kuwa kutokana na tukio hilo waliamua kuweka huduma ya uangalizi wa vyombo vya majini ili kuhakikisha kuwa vinafanyiwa uchunguzi kabla ya kuanza safari na kupewa kibali kutoka Sumatra.
Pia aliongeza kwa kusema kuwa abiria wa vyombo vya majini inabidi wapewe mafunzo ya kujiokoa pindi linapotokea tatizo na kusema kuwa mafunzo hayo inabidi wapewe mapema wanapo ingia ndani ya meli. Alisema kuwa mafunzo wanayotakiwa kupewa ni pamoja na jinsi ya kuvaa maboya,jinsi ya kutumia boti za ziada yanayokuwa ndani ya meli na njia nyingine mbadala ambazo zitaweza kuwasaidia watu katika kujiokoa.
Alimaliza kwa kuomba msaada wa vifaa ya kujiokolea
kutoa kwa moyo kama alivyoonyesha mfano Mwanamitindo Flaviana Matata
kwa kutoa maboya 500 ilikuweza kuwalinda wasafiri katika lolote
litakalojitokeza.
No comments:
Post a Comment