Dodoma.
Shirika la Umeme nchini (Tanesco), limepata hasara ya Jumla ya Sh966.18 milioni kutokana na wizi na uharibifu wa miundombinu katika mikoa mbalimbali nchini, Bunge lililezwa jana.
Shirika la Umeme nchini (Tanesco), limepata hasara ya Jumla ya Sh966.18 milioni kutokana na wizi na uharibifu wa miundombinu katika mikoa mbalimbali nchini, Bunge lililezwa jana.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa wizara hiyo kwa mwaka 2013/14.
Waziri huyo alisema, kiasi hicho ambacho ni sawa
na Dola za Marekani 603,862 kilipotea katika kipindi cha Julai 2012 hadi
Aprili 2013 ambapo ni hasara kubwa zaidi kwa Tanesco.
Kwa taarifa, ni wazi kuwa Tanesco imekuwa ikipata hasara ya karibu Sh96.7 milioni kila mwezi kiasi ambacho ni kikubwa.
“Wizi na uharibifu wa muda mrefu wa miundombinu ya umeme kwa muda mrefu umekuwa ni tatizo sugu kutokana na wahusika kubuni njia mbalimbali za kufanya uharibifu huo na kuisababishia Tanesco na nchi kwa ujumla hasara kubwa,” alisema Muhongo.
Akizungumzia tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa
mara, alisema, “Tatizo la kukatika kwa umeme ni uchakavu wa miundombinu
ya usambazaji na vifaa vyake pamoja na kuzidiwa uwezo kwa mifumo yake.”
Kingine alitaja kuwa ni wizi wa nyaya za shaba na mafuta ya transfoma zaidi kwenye mikoa ya Arusha,Kilimanjaro na Mkoa wa Tanga.
Alitaja mkakati wa kukabiliana na tatizo hilo kuwa
ni pamoja na kubadilisha nguzo zilizoharibika katika njia za msongo wa
Kv 0.4 na Kv 11 na 33, kukata miti na kubadilisha vikombe vilivyovunjika
na nyaya chakavu.
Waziri alitaja miradi mingi ya umeme ambayo wizara inajiandaa kuikamilisha katika maeneo mbalimbali nchini kuwa itagharimu fedha nyingi.
Miradi hiyo ni ile ya MCC, REA ambayo inaendelea
kuzinduliwa katika maeneo tofauti na mingi imetekelezwa kwa kiwango cha
kuridhisha.
Kwa upande wao Kambi ya Upinzani waliitaka Wizara ya Nishati na Madini kueleza ukweli kuhusu mgao wa umeme ambao unaendelea kuwatesa Watanzania huku kukiwa na taarifa kuwa hakuna mgao.
Akiwasilisha maoni ya kambi hiyo, Msemaji wa
Upinzani katika Wizara ya Nishati na Madini,John Nchimbi aliituhumu
Serikali kuwa imekuwa ikikanusha kuhusu mgao huo wakati hali ni tofauti
na kauli ya Serikali.
Kamati ya Nishati na Madini ilieleza kuwa katika kipindi cha
mwaka mmoja kuanzia Januari 2012 hadi Desemba 2012 jumla ya nyaya zenye
urefu wa kilomita 11.249 za thamani ya Sh408 ziliibwa.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Victor Mwambalaswa
alisema katika kipindi hicho pia mafuta ya trasnfoma ya thamani ya
Sh1.32 bilioni yaliibiwa katika transfoma 190 huku wateja 532
wakikamatwa kwa wizi wa umeme wenye thamani ya Sh5.6 bilioni.
No comments:
Post a Comment