Dar es Salaam.
Shirika la Kazi Dunia (ILO), limewataka waajiri wa wafanyakazi wa nyumbani kuwalipa mshahara wa Sh65,000 kama ilivyopitishwa na Serikali.
Shirika la Kazi Dunia (ILO), limewataka waajiri wa wafanyakazi wa nyumbani kuwalipa mshahara wa Sh65,000 kama ilivyopitishwa na Serikali.
Mkurugenzi wa ILO Tanzania, Alexio Musindo alisema licha ya wafanyakazi wa nyumbani kuwa na haki kama wengine kulipwa mshahara unaokidhi mahitaji, uzoefu unaonyesha wengi wao hubaguliwa na kunyanyaswa na waajiri.
Musindo alisema hatua hiyo inatokana na utii na ufuatiliaji mdogo wa sheria za kazi zilizopo.
Akizungumza kwenye ufunguzi wa semina ya wadau wa ajira jana, Musindo alisema kuna haja sasa
Serikali kuharakisha kuridhia mkataba wa kimataifa wa kazi namba 189. Mkurugenzi wa Jinsia ,Watoto na Vijana wa Chama cha Wafanyakazi wa Hifadhi, Hoteli, Nyumbani na Huduma za Jamii (Chodawu), Deograsia Vuluwa alisema wafanyakazi wa nyumbani wamekuwa wakinyimwa haki zao za msingi kwa muda mrefu.
Vuluwa alisema hiyo inatokana na sheria za kazi zilizopo kutoweka bayana masuala muhimu kama kima cha mshahara, mapumziko, likizo na likizo za uzazi.
Naye Mkurugenzi wa Ajira Wizara ya Kazi na Ajira,
Ally Msaki alisema kuna changamoto nyingi zinazokabili sekta ya ajira
kwa wafanyakazi wa nyumbani.
No comments:
Post a Comment