EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Sunday, May 19, 2013

MADAI MAZITO NISHA AHONGWA NYUMBA

Stori:Gladness Mallya-Global Publishers.
Unakumbuka zile habari za Wema Isaac Sepetu kununuliwa jumba la kifahari na bilionea mmoja Kijitonyama, Dar? Sasa zimegeukia kwa staa wa sinema za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ ambaye naye kuna madai mazito ya kuhongwa nyumba.
Ilikuwa mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo gazeti hili lilipokea ujumbe mfupi wa simu ya mkononi ‘sms’ kutoka kwa chanzo chake.
HABARI ILIVYOANZA
Chanzo: Hivi ninyi mna habari?
Risasi Jumamosi: Nyingi tu lakini kama una ya kwako itatufaa sana.
Chanzo: Kwa taarifa yenu Nisha kanunuliwa bonge la mjengo hapa Kijitonyama karibu kabisa na Kituo cha Polisi cha Kijitonyama ‘Mabatini’.
Risasi Jumamosi: Nani kamnunulia?
Chanzo: Nasikia ni bilionea mmoja mwenye fedha zake hapa Dar es Salaam, kainunua kisha kamhonga Nisha kwa sababu ni mpenzi wake.
Risasi Jumamosi: Tunashukuru kwa taarifa, kaa mkao wa kula itaruka hewani mara moja baada ya upelelezi wetu.
RISASI LATUA KIJITONYAMA
Baada ya kuzinyaka habari hizo, gazeti hili lilisaga soli hadi maeneo hayo na kuanza kugonga geti moja baada ya lingine hadi lilipofanikiwa kuinasa nyumba hiyo huku Nisha akiwa ndani kapumzika.
Msichana aliyejitambulisha kuwa ni dada wa kazi au hausigeli kwa lugha laini ndiye aliyetoboa siri kuwa ni kweli staa huyo yupo ndani na amehamia mahali hapo muda si mrefu.
RISASI LAINGIA MJENGONI
Risasi Jumamosi liliomba kukaribishwa ndani ili kupata ‘ditelzi’ na ndipo Nisha akaamka na kuamua kuacha paparazi wetu apige picha japo awali alitia ngumu akidai hayuko tayari kuianika nyumba hiyo.
Ndani ya nyumba hiyo yenye vyumba vitano, sebule, jiko, choo na mabafu mawili, anayeishi Nisha na dada wake wa kazi, kuna samani nyingi za bei mbaya, mazagazaga kibao, mazulia na marumaru huku kila kona kukiwa na Tv ya flat screen hadi chooni (angalia picha Uk.1).
 
NISHA ABANWA KUHUSU UMILIKI
Nisha anayemiliki kampuni ya kuzalisha muvi za Kibongo ya Nisha’s Film Production alipotakiwa kueleza kama kanunua, kanunuliwa au kapangisha nyumba hiyo, alikuwa na haya ya kusema:
“Ni juhudi zangu binafsi jamani, kujituma sana kwenye kazi yangu ya filamu. Kuhusu kununua au kupangisha naomba nikimaliza ‘process’ f’lanif’lani ndipo nitaweka wazi, kwa sasa bado ni mapema mno.”
Risasi Jumamosi: Kuna madai kuwa umehongwa hii nyumba na bilionea mmoja wa hapa Dar, je, ni kweli?
Nisha: Hakuna kitu kama hicho jamani, hayo ni maneno ya watu wasiojituma kufanya kazi kwa bidii. Haya ni matunda ya kufanya kazi sana.
Risasi Jumamosi: Nyumba hii ina samani mpya zote za thamani kubwa sana, je, zimegharimu fedha kiasi gani?
Nisha: Vitu vyote vya ndani hadi nikahamia vimegharimu karibu Sh. milioni 95. Ni fedha zilizotokana na mauzo ya filamu zangu nne nilizotengeneza mwenyewe mwaka jana.
Risasi Jumamosi: Kuna madai kuwa umejiunga Freemason ndiyo maana ndani ya kipindi kifupi mambo yako safi, je, ni kweli?
Nisha: Nimesikia hizo tetesi za Freemason ‘but’ naamini mti wenye matunda ndiyo hupigwa mawe. Mimi namwachia Mungu, namuomba kila siku anipe baraka zake, namshukuru na nazidi kumuomba nifanikiwe.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate