MREMBO aliyekuwa amevaa namba 9 kwenye shindano la kumsaka Redds Miss Ustawi 2013, Severine Emmanuel, juzikati aliibuka kidedea baada ya kuwamwaga washiriki 10, aliyokuwa akichuwana nao kuwania taji hilo.
Tukio hilo lilifanyika usiku wa kuamkia leo ndani ya Ukumbi wa Sun Cirro Shekilango jijini Dar es Salaam, likiratibiwa na majaji watatu ambao ni Sauda Mwilima, Salima Dakota na Michael Malus
Baada ya nafasi ya kwanza kwatawliwa na Severine Emmanuel nafasi ya pili alishika Cecilia Francis huku namba tatu ikitua mikononi mwa Angela Evarist, Doreen Martin aking’ang’ania nafasi ya nne na Phina Shebila akikamilisha nafasi ya tano Bora.
Habari/Picha: Musa Mateja/GPL
No comments:
Post a Comment