MATOKEO ya kidato cha nne ambayo serikali iliagiza yapitiwe upya
na kufanyiwa uhakiki kwa vigezo vya miaka ya nyuma, yametolewa jana
huku kukiwa na mabadiliko kidogo.
Matokeo hayo mapya yalionyesha hali bado ni mbaya kwani ni watahiniwa
30,000 tu kati ya 240,909 waliopata daraja sifuri ndiyo walionufaika na
‘mbeleko’ ya serikali.
Mabadiliko hayo yanaonyesha waliopata daraja sifuri wamepungua kidogo na sasa wamefikia 210,846.
Waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru
Kawambwa.
Matokeo yanaonyesha kiwango cha ufaulu kimeongezeka kwa asilimia 9
ambapo mara ya kwanza ilikuwa asilimia 34.5 wakati hivi sasa ni asilimia
43.08.
Matokeo hayo mapya yanaonyesha kuwa takriban asilimia 61 ya watahiniwa
walipata daraja sifuri awali sasa yamepungua na kuwa asilimia 56.9.
Akitangaza matokeo hayo kwa waandishi wa habari jana jijini Dar es
salaam, Waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru
Kawambwa, alisema hali bado ni mbaya.
Kawambwa alisema kuwa jumla ya watahiniwa 480,029 walisajiliwa kufanya
mtihani wa kidato cha nne mwaka jana wakiwemo wasichana 217,587 sawa
na asilimia 45 .33 na wavulana 262,442 sawa na asilimia 54.67.
Alisema watahiniwa waliofanya mtihani ni 458,139 sawa na asilimia
95.44 ambapo watahiniwa 21,890 sawa na asilimia 4.56 ya watahiniwa wote
waliosajiliwa hawakufanya mtihani kutokana na sababu mbalimbali.
Alibainisha kuwa matokeo ya watahiniwa wa shule 159,609 kati ya
watahiniwa 397,138 waliofanya mitihani walifaulu ambapo wasichana
walikuwa 60,751 na wavulana walikuwa ni 98,858.
Kawambwa alisema ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata
watahiniwa wa shule unaonyesha jumla ya watahiniwa 35,349 wamefaulu
katika daraja la 1-111 ambapo kati yao wasichana ni 10,924 na wavulana
ni 24,425 sawa na asilimia 43.08.
Matokeo ya awali yaliyotangazwa yalionyesha kuwa kati ya watahiniwa
367,756 waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana, waliokuwa
wamefaulu kwa daraja la kwanza mpaka la tatu walikuwa 126,847 sawa na
asilimia 6.4. Waliopata daraja la nne walikuwa ni 103,327 sawa na
asilimia 28.1.
Idadi ya watahiniwa waliotangazwa hapo awali na waliotangazwa sasa
imeonyesha pia kuwa na tofauti ambapo awali waziri alisema kuwa jumla
ya watahiniwa 35,349 wamefaulu katika madaraja 1-111 ambapo kati yao
wasichana ni 10,924 na wavulana ni 24,425.
Aliongeza kuwa katika matokeo hayo watahiniwa wa kujitegemea
waliosajiliwa walikuwa 68,804 wakiwemo wasichana 34,605 sawa na asilimia
50.30 na wavulana 34,199 sawa na asilimia 49.70 ambapo alisema
watahiniwa 61,001 wakiwemo wasichana 30,918 na wavulana 30,083
wamefanya mitihani wakati watahinmiwa 7,803 sawa na asilimia 11.34
hawakufanya mitihani.
Alzitaja shule za sekondari zilizoshika nafasi ya kumi katika kundi la
shule zenye watahiniwa 40 na zaidi ni shule ya wasichana St. Fransic
iliyoko Mbeya, Marian Pwani (Wavulana) na Feza Boys Dar es Salaam.
Shule nyingine ni Canosa, Feza Girls, Rosmini Girls, Anwarite Girls, St. Marys Mazinde Juu na Jude Moshono.
Pia alisema matokeo ya kupangiwa shule watakazotakiwa waende
yatafanyika mwezi Juni na wanafunzi wataanza kidato cha sita mwezi
Julai.
“Tumefanya hivyo, hatukuchakachua na matokeo haya ni halali kabisa
hivyo ndiyo yatakayokuwa rasmi kutumika sehemu yoyote na si yale ya
awali kama ilivyokuwa mwanzo,” alisema Waziri Kawambwa.
Shule watakazopangiwa
Kawamba alisema watahiniwa hao watapangiwa shule watakazotakiwa
waende kuanzia kesho na wanafunzi wataanza kidato cha sita mwezi ujao.
“Tumefanya hivyo hatukuchakachua na matokeo haya ni halali kabisa
hivyo ndiyo yatakayokuwa rasmi kutumika sehemu yoyote na si yale ya
awali,” alisema Kawambwa.
Alisema pia baada ya kufanya kwa marekebisho hayo ufaulu umeongezeka
kutoka asilimia 34.5 awali na sasa 43.08 huku akieleza kuwa mwaka 2001
matokeo yalikuwa juu kwa asilimia 53.
Hata hivyo alisema kuanzia sasa utatumika mfumo mpya ambapo alama zote
zitakuwa sawasawa na hakutakuwa na tofauti za alama katika masomo.
Kwa maelezo zaidi soma tangazo ukurasa wa 20
No comments:
Post a Comment