MAZOEZI
kwa ajili ya kujiandaa na shindano la kumsaka malkia wa kitongoji cha
Kigamboni mwaka huu "Redd's Miss Kigamboni 2013" yanatarajiwa kuanza
kufanyika kuanzia Jumatatu Mie 6 mwaka huu kwenye ukumbi wa Break Point
uliopo Posta jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na gazeti hili jana jijini, Mratibu wa shindano hilo, wa kampuni ya
K& L Media Solutions, Somoe Ng'itu, alisema kuwa maandalizi ya
shindano hilo yanaendelea na bado nafasi iko wazi kwa wasichana wote
wenye sifa za kushiriki shindano hilo kutoka sehemu mbalimbali hapa
nchini.
Mratibu
huyo alisema kwamba lengo la kuweka wazi na kuwahamasisha warembo ni
kutaka kutoa nafasi kwa wasichana wengi zaidi kujiandikisha na hatimaye
kupata mshindi atakayekiwakilisha vyema kitongoji hicho katika
mashindano ya ngazi ya Kanda yatakayofanyika baadaye mwezi ujao.
"Kila
kitu kinaendelea vizuri na kamati ya maandalizi imewataka wadau wa
sanaa ya urembo kujiandaa kuona mwaka huu shindano likiwa lenye ubora na
mvuto," alisema Somoe.
Aliongeza kwamba fomu kwa ajili ya kushiriki shindano hilo zinapatikana bure na washiriki ambao wako tayari wanaombwa kufika siku ya Jumatatu ili kuanza mazoezi.
Aliongeza kwamba fomu kwa ajili ya kushiriki shindano hilo zinapatikana bure na washiriki ambao wako tayari wanaombwa kufika siku ya Jumatatu ili kuanza mazoezi.
Alisema
pia makampuni na taasisi mbalimbali zinakaribishwa kudhamini shindano
hilo ambalo mwaka jana lilitoa mshindi katika kinyang'anyiro cha Kanda
ya Temeke ambaye ni Edda Sylivester.
Edda alifanikiwa kushika nafasi ya tatu kwenye fainali za taifa huku mshindi wa taifa ni Brigitte Alfred ambaye mwaka huu ataenda kupeperusha bendera ya nchi katika mashindano ya dunia.
Edda alifanikiwa kushika nafasi ya tatu kwenye fainali za taifa huku mshindi wa taifa ni Brigitte Alfred ambaye mwaka huu ataenda kupeperusha bendera ya nchi katika mashindano ya dunia.
Chanzo cha habari na BIN ZUBERY
No comments:
Post a Comment