Kocha wa Real Madrid Jose Mourinho, amesema huenda asiwe kocha wa klabu hiyo msimu ujao.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka hamsini, ambaye
amewahi kuongoza Chelsea, siku ya Jumanne, alishuhudia vijana wake
wakiondolewa kwenye nusu fainali ya michuano ya kuwania kombe la klabu
bingwa barani Ulaya, licha ya kuilaza Borussia Dortmund ya Ujerumani,
kwa magoli mawaili kwa yai.
Dortmund ilifuzu kwa fainali ya kombe hilo kwa jumla ya magoli manne kwa matatu.
Katika mechi ya raundi ya kwanza Dortmund, iliilaza Real Madrid kwa magoli manne kwa moja.
Kumekuwa ya ripoti kuwa kocha huyo kutoka Ureno,
alikuwa akijiandaa kukihama klabu hiyo ya Real Madrid na kurejea nchini
Uingereza.
Baada ya kumalizika kwa mechi hiyo ya jana
Morinho alisema , anafahamu kuwa anapendwa na mashabiki na vilabu vingi
nchini Uingereza.
Hata hivyo amesema atasalia hadi mwisho wa msimu huu kabla ya kuamua hatma yake ya siku zijazo.
Mourinho alikihama klabu ya Chelsea, katika hali
ambayo haikufahamika Septemba mwaka wa 2007, baada ya kutofautiana na
mmiliki wa klabu hiyo Roman Abramovich.
No comments:
Post a Comment