Moshi.
Vyombo vya ulinzi na usalama Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia), vimemtia mbaroni raia wa Nigeria akiwa amebeba kilo saba za dawa zinazoaminika ni za kulevya.
Vyombo vya ulinzi na usalama Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia), vimemtia mbaroni raia wa Nigeria akiwa amebeba kilo saba za dawa zinazoaminika ni za kulevya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz alisema raia huyo wa Nigeria alikamatwa saa 8:00 usiku wa kuamkia juzi, akijiandaa kuingia katika jengo la uwanja huo.
Boaz alisema mtuhumiwa huyo ambaye amejitambulisha
kuwa ni mfanyabiashara, alikuwa asafiri kwenda Ouagadougou kupitia
Adiss Ababa kwa ndege ya Shirika la Ethiopian Airline.
“Wakati anaingia pale uwanjani alipekuliwa na kukutwa na kilo saba za dawa za kulevya zikiwa zimefichwa katika mabegi yake manne ya kusafirikia,” alisema Boaz.
Kamanda Boaz alisema uchunguzi wa kina kubaini
aina ya dawa hizo unaendelea, lakini uchunguzi wa awali unaonyesha unga
huo ni dawa za kulevya.
No comments:
Post a Comment