Kubaini kuwa walitengeneza mtandao huo wa kuvusha mali kupitia bandari bubu zisizo rasmi maeneo ya Kawe hadi Bagamoyo.”
Alisema polisi kupitia teknolojia ya kisasa iliwabaini askari hao kwa nyakati mbalimbali wakishirikiana na wafanyabiashara hao ambao walikuwa wakitoa rushwa ili wasikamatwe.
“Mpaka sasa askari wa vyeo mbalimbali waliokamatwa wako 16 na wanaendelea kuhojiwa... majina yao yanahifadhiwa kwa sasa kwani bado kuna wengine wanatafutwa ili kuwabaini na kuusambaratisha mtandao mzima,” alisema.
Alisema mtu yeyote ambaye amefanya kosa ndani ya Jeshi la Polisi atachukuliwa hatua za kisheria na kufikishwa mahakamani kama raia wengine.
Kamanda Kova alisema operesheni hiyo itawalenga
wafanyabiashara, wafanyakazi wa TRA na wa taasisi nyingine
watakaobainika kuhusika na mtandao huo.
No comments:
Post a Comment