Katika hali ya kushangaza, mwanaume mwenye asili ya Kiarabu aliyetambulika kwa jina la Karina Mohamed (20), aliwaacha midomo wazi madaktari, wauguzi na wagonjwa wa Hospital ya Amana, jijini Dar baada kulazwa katika wodi ya wanawake akidhaniwa ni mwanamke.

Chanzo
chetu kilizidi kueleza kwamba baada ya mgonjwa huyo kupelekwa wodini,
hakuna hata mgonjwa mmoja aliyeweza kumtambua kuwa ni mwanaume kutokana
na maumbile yake kufanana kabisa na ya kike lakini wakati madaktari
wakiendelea kumhudumia, Aprili 25 akafariki dunia.
Imeelezwa kuwa baada ya kuzidiwa sana, mhudumu wa hospitali hiyo alipotaka kumuwekea mpira kwa ajili ya kujisaidia haja ndogo ndipo aliposhtuka baada ya kubaini kuwa ana jinsia ya kiume tofauti na alivyodhania.

“Kitendo
kile kilimshangaza sana muuguzi huyo na kudondosha kila kitu alichokuwa
nacho mkononi huku akisema: Huyu mgonjwa mwanaumeee jamani.”
Mara baada ya waandishi wetu kupewa taarifa, walifika hospitali hapo na kuonana na katibu wa hospitali hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Tunu Mwachali ambaye alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa suala hilo lipo mikononi mwa polisi.

Kamanda wa Polisi, Mkoa wa
Kipolisi Ilala, Marietha Minangi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na
kudai kuwa mgonjwa huyo alifikishwa hospitalini hapo Aprili 24, mwaka
huu na kulazwa wodi namba 2 ya wanawake na kufariki dunia akiwa
anapatiwa huduma na kuongeza kuwa ndugu zake bado hawajafahamika ila
jeshi linaendelea na uchunguzi.
No comments:
Post a Comment