
BAADA ya uvumi kwamba msanii wa muziki wa kizazi kipya wa Kenya Prezo
kuzama kwenye mahaba mazito na msanii wa filamu nchini Tanzania Wema
Sepetu, Msanii huyo ameshikwa na kigugumizi na kushindwa kukanusha
tuhuma hizo.
Prezo ambaye alifiwa na mchumba wake ambaye pia alikuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Nigeria marehemu Goldie Harvey, aliyefariki dunia February mwaka huu, juzi alishindwa kudhibitisha tuhuma hizo baada ya kuulizwa swali na kushindwa kulijibu.
Prezo ambaye yuko nchini kwa ziara ya muziki alionekana katika picha za mahaba akiwa na Wema Sepetu, hata hivyo Wema aliwahi kukanusha picha hizo na kudai kwamba walipiga wakati walipokuwa wakirekodi filamu mpya ya Wema na kwamba hana mahusiano yoyote ya mapenzi na msanii huyo.Endelea kusoma zaidi hapa chini...
Akiwa katika mahojiano maalum kwenye kipindi cha mapenzi
kilichorushwa usiku na Redio Clouds FM Prezo alishikwa na kwi kwi cha
gafla baada ya kutakiwa kudhibitisha juu ya uvumi kwamba amenasa kwenye
mahaba mazito na mrembo huyo mwenye skendo za kubadilisha wanaume kila
kukicha.
Mtangazaji wa kipindi hicho, Loveness maarufu kwa jina la Diva
alimtaka Prezo kuweka bayana juu tuhuma hizo, hata hivyo Prezo
alishindwa badala yake akaanza kujing'ata ng'ata huku akipotezea swali
hilo kwa kuingiza bada nyingine.
"Prezo twambie kuhusu mahusiano yako wewe na Wema Sepetu, kuna
uvumi kwamba umezama kwenye mapenzi yake je hili lina ukweli gani?"
aliuza Diva, hata hivyo baada ya swali hilo Prezo alitoka nje ya swali
na kuzungumzia masuala mengine kwa lengo la kukwepa kutoa jibu, hata
alipoulizwa tena kwa mara ya pili na yatatu, Prezo akasema bado
unaulizwa swali hilo hepu tuliache.
Kitendo cha Prezo kushindwa kujibu swali hilo ni ishara kwamba
wawili hao wameanza kuimarisha mahusiano yao na kwamba wasinge penda
kulizungumzia kwani bado ni mapema sana.
No comments:
Post a Comment