BAO
la Ben Watson katika dakika ya mwisho kabisa jioni hii limeipa Wigan
ubingwa wa Kombe la FA kwa mara ya kwanza kabisa ikiichapa Manchester
City 1-0 kwenye Uwanja wa Wembley.
Nyota
huyo aliyetokea benchi alifunga kwa kichwa akiunganisha kona na kuwa
shujaa wa mashabiki wa Wigan na kumfanya Roberto Mancini arejee nyumbani
mikono mitupu.
Man City ilimaliza pungufu ya mchezaji mmoja baada ya Zabaleta kutolewa nje kwa kadi nyekundu daika ya 84.
Katika mchezo huo, kikosi cha Man City kilikuwa: Hart, Zabaleta, Kompany, Nastasic, Clichy, Silva, Toure , Barry/Dzeko dk90, Nasri/Milner dk54, Aguero na Tevez/Rodwell dk69.
Wigan: Robles, Boyce, Scharner, Alcaraz, Espinoza, McCarthy, McArthur, Gomez/Watson dk81, McManaman, Kone na Maloney.
Joe Hart akiruka bila mafanikio
Mancini sasa anaweza kutimuliwa Manchester City akimpisha kocha wa Malaga, Manuel Pelligrini
Sergio Aguero akijutia kupoteza nafasi ya kufunga
Dua iliyopokewa: Wachezaji wa Wigan wakiomba dua kabla ya mechi
Shabiki wa Manchester City akifurahia na Kombe bandia kabla ya mechi
Mashabiki wawili wa Manchester City wakiwa wamevaa sura bandia za Mancini leo Wembley
Kombe halisi: Kombe la FA likiwasilishwa uwanjani
No comments:
Post a Comment