WACHEZAJI wa timu ya Taifa, Taifa Stars jana walikabidhiwa Milioni 30,
ikiwa ni pongezi ya kufanya vizuri dhidi ya Zambia na Morocco, huku
wakiwatakiwa kuhakikisha wanashinda mechi ya marudiano dhidi ya Morocco.
Akizungumza jijini juzi, wakati wa kukabizi fedha
hizo kwa wachezaji, Mwenyekiti wa Kamati ya ushindi ya Taifa Stars, Mohammed
Dewji alisema timu hiyo inastahili pongezi kwa juhudi iliyoweza kuonyesha.
Dewji alisema wachezaji wameweza kurudisha heshima
ya Tanzania, huku akiwataka wahakikishe
wanaonyesha nidhamu ya hali ya juu ili wafanikiwe zaidi.
“Nidhamu itasaidia timu yetu kufika mbali zaidi ya
hapa, kila mchezaji anatakiwa kuwa na jukumu kujituma zaidi ya mwingine ili
tutaweze kufikia malengo yetu,” alisema
Alisema ni vizuri kila mchezaji wa timu hiyo,
akawaza mpira zaidi ya kitu kingine, ili kujiongezea uwezo wa kufikiri na mbinu
mbalimbali za kusaidia timu yake.
“Inatakiwa kuanzia sasa, wachezaji wote wawaze
mpira, vizuri ukilala na kuamka ukawaza jinsi gani utaweza kuisaidia nchi yako
na kuifanyia makubwa kupitia soka,”alisema
Mwenyekiti huyo alisema mbali na fedha hizo
waliozotoa, Kamati hiyo itaendelea kusaidia timu hiyo ili iweze kufanikiwa,
huku kila kiongozi akiwa amepewa majukumu yake.
Katika hatua nyingine, kocha wa timu hiyo Kim Poulsen
alisema anaimani kikosi chake alichokichagua
kitafanya vizuri, kwani ameshaona mwangaza huo katika mechi mbalimbali
walizocheza.
Timu hiyo ipo kambini kwa ajili ya maandalizi ya
kuelekea Morocco katika mchezo wake wa marudiano utakaofanyika Julai mwaka huu,
huku ikitarajiwa kujipima nguvu dhidi ya Sudan
nchi Ethiopia kabla ya kuvaana na
Morocco.
Taifa Stars, iliweza kuibuka na ushindi hapa
nyumbani kwa kuifunga Morocco bao 3-1, mechi hiyo ikiwa ni kuwania kufudhu
kucheza kombe la dunia mwakani .
No comments:
Post a Comment