Waombaji waliotuma maombi ya fursa za ajira kwa ajili ya matangazo 
yaliyokuwa yametolewa na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma  
kwa niaba ya Waajiri mbalimbali nchini mnamo  tarehe 26 Machi, 2013 moja
 likiwa katika lugha ya Kiingereza na lingine katika lugha ya Kiswahili 
ambapo mwisho wa kutuma maombi ilikuwa tarehe 9 Aprili, 2013 wametakiwa 
kutembelea tovuti ya 
Sekretarieti ya Ajira mara kwa mara ili kupata 
ratiba ya usaili kwa nafasi walizoomba.
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Bw. Xavier Daudi amesema hayo leo alipokuwa akiongea na baadhi ya wadau waliomtembelea ofisini kwake wakitaka ufafanuzi wa masuala mbalimbali yanayohusu mchakato wa Ajira Serikalini.
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Bw. Xavier Daudi amesema hayo leo alipokuwa akiongea na baadhi ya wadau waliomtembelea ofisini kwake wakitaka ufafanuzi wa masuala mbalimbali yanayohusu mchakato wa Ajira Serikalini.
Amesema ofisi yake itaendelea kuwafahamisha 
wale wote walioomba  nafasi za kazi Serikalini kadri siku zinavyosogea. 
Amebainisha kuwa kwa tangazo la kiingereza lililotolewa tarehe 26 Machi,
 2013 ambalo lilihusu Taasisi za Umma  zaidi, usaili wake utaanza tarehe
 20 mwezi huu kama ratiba ilivyoainisha katika tangazo la kuwaita kwenye
 usaili lililotolewa tahere 16 Mei, 2013 kupitia tovuti ya Sekretarieti 
ya Ajira likibainisha usaili utafanyika tarehe ngapi na sehemu gani 
pamoja na orodha ya majina ya wahusika waliokidhi vigezo vya tangazo 
kwa  nafasi hizo.
Daudi  amewataka waombaji wa tangazo lililokuwa
 limetolewa kwa lugha ya Kiswahili tarehe tarehe 26 Machi, 2013 
waendelee  kuvuta subira kwani ratiba yake ya Usaili kwa waombaji wenye 
Sifa itatolewa mara baada ya Usaili wa Tangazo la Kingereza kukamilika 
ili kuepuka kuwachanganya waombaji. Pamoja na hayo amewataka waombaji 
hao kukaa tayari kwani usaili wa tangazo hilo unaweza kufanyika wakati 
wowote mwezi Juni mwaka huu ila tarehe rasmi na wapi watajulishwa 
baadae.
Aidha, Waombaji wa nafasi wazi za kazi  kwa 
tangazo la kazi lililotolewa kupitia tovuti hii tarehe  16 Aprili, 2013 
ambalo mwisho wake wa kutuma maombi ilikuwa tarehe 2 Mei, 2013,  
wanafahamishwa kuwa mchakato wa kuchambua maombi yao bado unaendelea na 
watapewa taarifa ya kuitwa kwenye usaili kwa wale waliokidhi vigezo vya 
tangazo mara baada ya taratibu zote kukamilika.
Katibu huyo pia ametoa Rai kwa waombaji wote 
waliochaguliwa kuja kufanya usaili kujiandaa vyema ikiwa ni pamoja na 
kuzingatia vitu muhimu wanavyopaswa kuja navyo kwenye usaili ikiwemo 
vyeti vya Kitaaluma.
 
Daudi alimalizia kwa  kuwatahadharisha waombaji 
wa fursa za Ajira serikalini pamoja na wadau  kuwa makini na baadhi ya 
Matangazo ya Ajira ambayo yanatolewa kupitia baadhi ya mitandao ya 
kijamii hususani wa  www.eastafricajobscareer.com
 yenye lengo la kupotosha jamii. Ofisi yake imefikia hatua ya kusema 
haya kutokana na mtandao huo alioutaja hapo juu kuchukua matangazo ya 
taasisi yake na kuyabadilisha tarehe za kutolewa, mwisho wa kutuma 
maombi, kumbukumbu namba pamoja na vichwa vya habari na kuyaweka hewani 
ilihali wakijua wazi hayajatolewa na Sekretarieti ya Ajira.
Hivyo amewataka wadau wote kuyapuuza matangazo 
hayo ya uongo yenye nia ya kuwapotosha. Aidha, amewahimiza wananchi 
pindi wanapoona matangazo ya kazi yanayoihusisha Sekretarieti ya Ajira 
katika Utumishi wa Umma katika mitandao au mbao za matangazo 
kujiridhisha ili kuyathibitisha kupitia  tovuti ya www.ajira.go.tz ili kuwa na uhakika zaidi kuliko kudanganywa na kutuma barua za maombi kwa matangazo ambayo si ya kweli.
Imetolewa na  Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Ofisi ya Rais-Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
Kwa maelezo zaidi; wasiliana na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Kwa barua pepe; gcu@ajira.go.tz au simu 255-687624975
20 Mei, 2013
Ofisi ya Rais-Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
Kwa maelezo zaidi; wasiliana na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Kwa barua pepe; gcu@ajira.go.tz au simu 255-687624975
20 Mei, 2013
No comments:
Post a Comment