Mwanafunzi  wa chuo kikuu cha Dodoma  
anayejulikana  kwa jina  la Boid Mwakitalima  amefariki dunia  baada  
kugongwa na treni....Mwanafunzi huyo  alikuwa  mwaka  wa  tatu.
Taarifa zinaeleza kuwa, mwanafunzi huyo alikuwa anatembea pembezoni mwa reli huku akiwa ameweka "headphone" sikioni, hali iliyomfanya ashindwe kusikia ama kuhisi chochote juu ya muungurumo wa treni hilo mpaka lilipomsogelea karibu na kumsukuma pembeni ambapo aliangukia chuma na kuaga dunia pale pale...
 Makamu Mkuu wa Chuo kikuu  cha Dodoma Prof.Idrisa Kikula  akiwasili Collage ya Informatics
 Mbele  ni Mshauri wa wanafunzi ( dean of student) chuo kikuu cha dodoma, Nyuma ni mshauri wa wanafunzi, Pro.Anatory  ( dean of students)  collage ya informatics na Katikati ni Makamu mkuu wa chuo cha Dodoma...
Baada  ya  ajali  hiyo, 
mwanafunzi  huyo  alipelekwa  chumba  cha kuhifadhia  maiti  katika  
hospitali  ya  Mkoa  wa Domoma, "General hospital" ambapo  leo  hii  
ameagwa  na wanafunzi wenzake  wa  chuo  kikuu  cha Dodoma  na  
kusafirishwa  kwenda  nyumbani  kwao Mbeya kwa  mazishi.
 Wanafunzi wakiuaga  mwili  wa  marehemu  kwa  huzuni
 Mkuu wa  collage ya Informatics, Prof. Mvuma,  akitoa  nasaha  zake
 Rais  wa wanafunzi, collage ya informatics  akitoa  nasaha  zake












No comments:
Post a Comment