Dodoma.
Upepo wa kisiasa hapa nchini unaonyesha kuwa hakuna uwezekano wa Tanzania kuwa na rais mwanamke mwaka 2015.
Upepo wa kisiasa hapa nchini unaonyesha kuwa hakuna uwezekano wa Tanzania kuwa na rais mwanamke mwaka 2015.
Rais Jakaya Kikwete anatarajia kung’atuka mwaka 2015 na kuacha nafasi hiyo kuchukuliwa na mtu mwingine ambaye atashinda kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka huo.
Wabunge mbalimbali waliohojiwa kwa nyakati tofauti
na gazeti hili, wamesema kuwa mwanamke hana nafasi hiyo kwa sasa, labda
iwe ni nguvu mpya itakayochochewa na Katiba Mpya inayoandaliwa.
Mbunge wa Gando (CUF), Khalifa Suleiman Khalifa alisema ni kujidanganya kabisa kwa mtu kusema kuwa Tanzania inaweza kuwa na rais mwanamke 2015.
Alisema pamoja na kuwapo na nguvu kubwa ya
kuwasukuma wanawake kujongea nafasi za juu kisiasa na kiserikali nchini,
hakuna ambaye ameonyesha nguvu za waziwazi kisiasa.
Alisema mfumo dume ambao upo nchini kwa sasa ni kikwazo kingine ambacho hakitoi nafasi kwa mwanamke atakeyegombea kuweza kushinda nafasi hiyo.
Alisema mazingira yanaonyesha chama chochote cha
siasa kilichodhamiria kushinda ni vigumu kumsimamisha mwanamke kwa
sababu itabidi kitumie nguvu kubwa ya ushawishi ili akubalike na
achaguliwe.
Kwa sababu hiyo, akasema hata wanawake wenye moyo na nia ya kukalia kiti hicho watapata vikwazo kuanzia kwenye vyama vyao hadi kwa wananchi.
“Ili mwanamke aweze kupitishwa na chama chake agombee urais, ni lazima kwanza yeye mwenyewe aonyeshe mvuto kwa umma kiasi cha kushawishi hata chama chake kiamini kuwa kitakuwa na kazi nyepesi ya kumnadi,” alisema Khalifa.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
Profesa Anna Tibaijuka alikiri kuwa hadi sasa hakuna picha ya moja kwa
moja inayoashiria kuwa 2015 mwanamke anaweza akachukua kiti cha urais.
Alisema hiyo inatokana na ukweli kwamba hakuna ambaye amejitokeza waziwazi lakini akasema wenye uamuzi wa kufanya hivyo ni wananchi.
Hata hivyo, alisema tangu Rais Jakaya Kikwete
aingie madarakani mwaka 2005, amekuwa akifanya juhudi za makusudi katika
kuhakikisha wanawake wengi wanapewa nafasi za juu katika ngazi za
kisiasa na kiserikali.
Alisema ingawa kwa sasa hakuna mwanamke ambaye ameonekana waziwazi kutaka kugombea nafasi hiyo, lakini anaamini kwamba juhudi za Rais Kikwete zimekuwa ni hatua moja ya kuwahamasisha wagombee nafasi hiyo.
Profesa Tibaijuka ambaye amewahi kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa, alisema mfumodume ndiyo umekuwa kikwazo kwa wanawake wengi kutojiamini hivyo kushindwa kujitokeza na kugombea nafasi za juu kama urais.
Alitoa mfano wa yeye mwenyewe ambaye alisema alipojitokeza kugombea katika jimbo la Muleba Kusini alijikuta ni mgombea pekee kutokana na chama cha Chadema kutamka wazi hawana haja ya kumsimamisha mgombea, hivyo wakawa wamemuunga mkono.
Profesa Tibaijuka ambaye amekuwa miongoni mwa wanawake ambao wameshika nafasi za juu kwenye nafasi za kimataifa, amekuwa miongoni mwa wanawake ambao wanatajwa wanaweza kuchukua kiti cha urais 2015.
Alipoulizwa kuhusu suala hilo, alisema “hiki ni kizazi kipya. Kizazi kinachohitaji mabadiliko. Ni vigumu mtu kusema tu anataka, bali chama husika nacho kina nafasi kubwa katika kushawishi.”
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka alisema anaamini kuwa mazingira yalivyo hivi sasa si rahisi kumpata rais mwanamke 2015, “labda kupitia Katiba Mpya inayoandaliwa sasa.”
Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema) Lucy Owenya alisema kipimo cha kujua kama kuna uwezekano huo, ni kuangalia wanawake mbalimbali waliopewa majukumu makubwa kama wamefanikiwa au la.
Kwa hali hiyo, alimwelezea Rais Kikwete kama mwanamapinduzi wa mapinduzi ya demokrasia kwa wanawake nchini.
Alisema ingawa kwa sasa hakuna mwanamke ambaye ameonekana waziwazi kutaka kugombea nafasi hiyo, lakini anaamini kwamba juhudi za Rais Kikwete zimekuwa ni hatua moja ya kuwahamasisha wagombee nafasi hiyo.
Profesa Tibaijuka ambaye amewahi kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa, alisema mfumodume ndiyo umekuwa kikwazo kwa wanawake wengi kutojiamini hivyo kushindwa kujitokeza na kugombea nafasi za juu kama urais.
Alitoa mfano kuwa bungeni kwa sasa wapo wanawake ambao wameshinda kupitia majimbo mbalimbali tena kwa kushindana na wanaume.
Alitoa mfano wa yeye mwenyewe ambaye alisema alipojitokeza kugombea katika jimbo la Muleba Kusini alijikuta ni mgombea pekee kutokana na chama cha Chadema kutamka wazi hawana haja ya kumsimamisha mgombea, hivyo wakawa wamemuunga mkono.
Profesa Tibaijuka ambaye amekuwa miongoni mwa wanawake ambao wameshika nafasi za juu kwenye nafasi za kimataifa, amekuwa miongoni mwa wanawake ambao wanatajwa wanaweza kuchukua kiti cha urais 2015.
Alipoulizwa kuhusu suala hilo, alisema “hiki ni kizazi kipya. Kizazi kinachohitaji mabadiliko. Ni vigumu mtu kusema tu anataka, bali chama husika nacho kina nafasi kubwa katika kushawishi.”
Mwanamke mwingine anayetajwa kuwa anaweza kuwa
Rais wa Tanzania ni Dk Asha Rose Migiro, aliyewahi kuwa Naibu Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa (2007 -2012), lakini mwenyewe hajawahi kusema
chochote kuhusu hilo.
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka alisema anaamini kuwa mazingira yalivyo hivi sasa si rahisi kumpata rais mwanamke 2015, “labda kupitia Katiba Mpya inayoandaliwa sasa.”
Hata hivyo hakupenda kufafanua zaidi juu ya suala hilo kwa kile alichoeleza ni hofu ya kunukuliwa vibaya.
Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema) Lucy Owenya alisema kipimo cha kujua kama kuna uwezekano huo, ni kuangalia wanawake mbalimbali waliopewa majukumu makubwa kama wamefanikiwa au la.
“Hicho ndicho kinatakiwa kiwe kipimo chetu. Mimi
sitaki kujadili majina ya watu hapa lakini mtu yeyote, hata wewe unaweza
kuchunguza,” alisema Owenya.
Alitoa mfano akisema mfumo wa uongozi wa nchi umekuwa ukijaribu kutoa nafasi za upendeleo kwa wanawake ili kuwapa moyo na uzoefu kwenye ngazi za uamuzi ili na wao wajiamini kuwa wana nguvu katika jamii. Pamoja na juhudi hizo alisema bado hakuna uthubutu wa wenyewe kujiamini na kutafuta madaraka ya juu kuanzia kwenye vyama hadi nafasi za juu za siasa katika nchi.
Hata hivyo, alisema anaamini wapo wengi ambao wamepata uzoefu mkubwa kimadaraka lakini hakuna ambao wameonyesha ushawishi mkubwa kisiasa kiasi cha kuwapa nafasi kubwa ya kushinda kirahisi 2015.
Mbunge wa Mjimkongwe (CUF), Muhammad Ibrahim Sanya alisema kwa hali ilivyo ni vigumu kwa mwanamke kuchukua kiti cha urais mwaka 2015.
“(Rais 2015) Hii ni ngumu! Ni ngumu! Lakini ‘nothing is imposible’ (hakuna kisichowezekana). Vyama vikidhamiria na wakawepo wanawake wenye uthubutu, dhamira na kujiamini, inawezekana,” alisema Sanya.
Alisema kuna nchi ambazo wanawake wameweza kuonyesha uwezo mkubwa wa kuongoza kama vile India, Pakistan, Malaysia na Uingereza, Ujerumani na hata Liberia.
Alikiri kuwa upepo wa kisiasa kwa sasa unatoa nafasi kubwa zaidi kwa rais mwanamume kwa kuzingatia umaarufu wa kisiasa pamoja na utamaduni ambao unaoupa nguvu mfumo dume.

Lakini alisema kuwa iwapo vyama vitadhamiria na
wakawepo wanawake ambao wanadhamira, wakajiamini na kuwa na uthubutu,
huenda itawezekana lakini kwa hali ilivyo sasa hatuoni jinsi jambo hilo
litakavyofanikiwa.
“(Rais 2015) Hii ni ngumu! Ni ngumu! Lakini ‘nothing is imposible’ (hakuna kisichowezekana). Vyama vikidhamiria na wakawepo wanawake wenye uthubutu, dhamira na kujiamini, inawezekana,” alisema Sanya.
Alisema kuna nchi ambazo wanawake wameweza kuonyesha uwezo mkubwa wa kuongoza kama vile India, Pakistan, Malaysia na Uingereza, Ujerumani na hata Liberia.
“Lakini ukichunguza kwa makini utakuta kuwa kuna msukumo uliotokana na vyama ambao umewafikisha hapo,” alisema Sanya.
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Lucy Mayenga alisema
kuna uwezekano wa 2015 Tanzania ikawa na rais mwanamke, ila
kinachotakiwa ni kuwapo na uthubutu na kujiamini.
Alikiri kuwa upepo wa kisiasa kwa sasa unatoa nafasi kubwa zaidi kwa rais mwanamume kwa kuzingatia umaarufu wa kisiasa pamoja na utamaduni ambao unaoupa nguvu mfumo dume.
Naye Mhadhiri wa Chuo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM),Richard Mbunda alisema, mwanamke akipewa nafasi anaweza
kulifikisha taifa mahali pazuri.
“Ni kweli kabisa mwanamke anaweza kuingoza nchi na
kuna mfano kama nchi ya Liberia inayoongozwa na Mwanamke (Rais Ellen
Johnson Sirleaf) inafanya vizuri,”alisema Mbunda na kuongeza:
“Hata hivyo, siyo sahihi kusema ni zamu ya
mwanamke kwani kufanya iwe zamu ya mwanamke na kujaribu kama majaribio
ni hatari kwa nafasi hiyo nyeti kwa taifa.”
Kwa upande wake Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Profesa
George Shumbusho alisema hafikirii kama ni wakati wa mwanamke au
mwanamume anaweza kuliongoza taifa.
“Tunachokitaka siyo mwanamke au mwanamume kuongoza
nchi, bali ni mtu makini na mwenye uwezo wa kuliongoza taifa,”alisema
Profesa Shumbusho .
Aliongeza: “Lakini kuna wanawake kama wawili,
watatu hivi wana uwezo wa kuongoza na nafikiri hivyo kwani urais ni
taasisi na wanaomsaidia wakitekeleza wajibu wao ipasavyo hakuna
litakaloshindikana.”
Mhadhiri wa UDSM, Dk Aneth Komba alisema: “Suala
ni kuwa na mtu anayeweza kutuongoza na kutufikisha tunapopataka, awe
mwanamke au mwanamume yote ni sawa na kama ni mwanamke ana uwezo ni
sawa, lakini siyo kusema ni awamu ya mwanamke.”
No comments:
Post a Comment