TAARIFA iliyotua kwenye dawati la gazeti hili hivi karibuni inaeleza
kuwa, mavazi yasiyo ya heshima vikiwemo vimini yamepigwa marufuku...
kuvaliwa na wasanii kwenye filamu wanazorekodi na yoyote atayekiuka atakiona cha mtemakuni.
Chanzo chetu makini kilichoomba hifadhi ya jina lake, kimeeleza kuwa
waliotoa agizo hilo ni Serikali ya Tanzania kupitia Bodi ya Filamu lengo
likiwa ni kuhakikisha maadili ya taifa yanazingatiwa.
Ikaelezwa
kuwa hatua hiyo imekuja kufuatia uwepo wa filamu nyingi mtaani ambazo
wasanii wanaoshiriki huvaa mavazi yasiyo ya heshima, mazingira
yanayoiharibu jamii.
“Kama wanavyosema vijana huko mtaani kwamba kimenuka na kweli kimenuka! Sasa hivi vimini ‘no’ kwenye filamu, bodi ya filamu imeona ilivalie njuga suala hili ili kulinda maadili ya taifa,” kilieleza chanzo hicho.
“Kama wanavyosema vijana huko mtaani kwamba kimenuka na kweli kimenuka! Sasa hivi vimini ‘no’ kwenye filamu, bodi ya filamu imeona ilivalie njuga suala hili ili kulinda maadili ya taifa,” kilieleza chanzo hicho.
Katika kujua ukweli wa jambo hili, mwandishi wetu alimtafuta Rais wa
Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba ambaye alikiri
kuwepo kwa utaratibu mpya wa Bodi ya Filamu wa kuzipitia filamu
zinazoingia mtaani na kwamba zinazokiuka maadili zinafungiwa.
Endelea kusoma ...
Mwakifwamba alisema ni kweli mavazi ya nusu utupu hayataruhusiwa tena
kuonekana kwenye filamu kama ilivyokuwa huko nyuma na wale
watakaojifanya vichwa ngumu watashughulikiwa.
“Sasa hivi kuna
sheria mpya kabisa, hakuna kuvaa nguo zisizo za maadili na ukikiuka basi
filamu yako haioneshwi au kama unaweza urudie na kuondoa vipande
vilivyoharibu filamu hiyo,” alisema Mwakifwamba huku kukiwa na maelezo
kuwa, hilo pia litasimamiwa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo chini ya Waziri Fenella Mukangara.
No comments:
Post a Comment