EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Tuesday, June 25, 2013

Afya ya Mandela yazidi kudorora

Pretoria. 
Ikulu ya Afrika Kusini imetoa taarifa kuwa hali ya Rais wake wa zamani, Nelson Mandela imezidi kuwa mbaya katika siku mbili zilizopita.

Taarifa hiyo ilithibitishwa na Rais Jacob Zuma ambaye kwa mara ya kwanza alikiri hadharani kwamba hali ya afya ya Mandela ni mbaya na madaktari wanaendelea na juhudi za kuokoa maisha yake.


Zuma ambaye pia ni Rais wa Chama cha African National Congress (ANC), alikiri kufadhaishwa na hali ya kiongozi huyo wa zamani, alipomtembelea katika Hospitali ya Magonjwa ya Moyo ya Medi-Clinic mjini Pretoria na kuzungumza na mkewe, Graca Machel kuhusu hali yake.

Kumekuwa na taarifa kwamba tangu alipofikishwa hospitali, Mandela amekuwa hajitambui na amekuwa akipumua kwa msaada wa mashine.


Pia, kumekuwa na ulinzi mkali katika hospitali hiyo alikolazwa huku waandishi wa habari na watu wasiokuwa wanafamilia wakizuiwa kwenda kumwona.

Ilielezwa pia kwamba ulinzi ulizidi kuimarishwa jana katika maeneo yanayozunguka hospitali hiyo.


ANC ambacho ndicho chama kinachotawala Afrika Kusini, pia kilitoa taarifa yake jana asubuhi kikielezea wasiwasi kuhusu afya ya kiongozi wake huyo wa zamani maarufu kwa jina la Madiba kuzidi kuwa mbaya.

Msemaji wa chama hicho, Jackson Mthembu aliwataka wananchi wa Afrika Kusini na dunia kwa jumla kuwaombea Mandela, ndugu zake na madaktari.


Hatua hiyo imesababisha simanzi na majonzi kwa wananchi wa Afrika Kusini ambao wamekuwa wakimwombea na kutoa salamu za kumtakia afya njema.

Mandela alilazwa katika Hospitali ya Moyo ya Medi-Clinic, Juni 8, mwaka huu kutokana na maradhi ya homa ya mapafu yanayomsumbua na iliripotiwa kwamba tangu wakati huo hajitambui.


Hatua ya Serikali kupitia Ofisi ya Rais Zuma kutangaza kwamba hali ya Mandela ni mbaya, imeongeza wasiwasi kwa wananchi na wengi wameitikia wito wa kuendelea kufanya maombezi maalumu kwa Mandela.

Hata hivyo, ofisa mmoja mwandamizi wa Serikali ambaye hakutaka kutajwa jina lake alisema kwa sasa hali ya Madiba si nzuri na kwamba wananchi wa Afrika Kusini wasiwe na matumaini kupita kiasi kuhusu kuimarika kwa hali ya afya yake.

Awali, wiki iliyopita Rais Zuma alisema madaktari wanafanya kila linalowezekana ili kuirejesha afya yake na kwamba anaangaliwa vizuri sana.
Zuma ambaye alieleza wasifu wa Mandela na kusema kwamba anaamini mpiganaji huyo hawezi kukubali kufa kirahisi alisema, madaktari wanafanya juhudi zote kumsaidia.
Pia alirejea kauli yake ya kulitaka taifa na dunia kumwombea apate nafuu. Vyombo vya habari nchini humo na hata vya kimataifa vilidai kwamba Mandela alizidiwa tena juzi usiku kiasi cha kushtua umati wa watu waliokuwa wakimwombea nje ya Hospitali hiyo.
Msemaji wa Ikulu ya Afrika Kusini, Mac Maharaj pia alisema hali ya Mandela ilikuwa ni mahututi.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate