BAO
la kichwa la Paulinho zikiwa zimesalia dakika nne kabla ya filimbi ya
mwisho, limeipa Brazil ushindi wa 2-1 dhidi ya Uruguay usiku huu na
kutinga Fainali ya Kombe la Mabara.
Maua mazuri: Mashabiki wa Brazi
Diego Forlan alikosa penalti dakika ya 13, baada ya beki wa Chelsea, David Luiz kumuangusha Diego Lugano kwenye eneo la hatari.
| |
Fainali
ya michuano hiyo 'amsha amsha' kuelekea Fainali za Kombe la Dunia,
itapigwa mjini Rio de Janeiro kwenye Uwanja wa Maracana Jumapili.
Brazil
ilibadilisha kikosi kutoka kile kilichoifunga Italia katika mechi yao
ya mwisho ya Kundi A, ikimuanzisha Paulinho badala ya Hernanes katika
kiungo.
Katika mchezo huo, kikosi cha Brazil kilikuwa; Julio
Cesar, Dani Alves, Thiago Silva, Luiz, Marcelo, Oscar/Hernanes dk72,
Gustavo, Paulinho, Fred, Hulk/Bernard dk64 na Neymar/Dante dk90.
Uruguay: Muslera, Lugano, Godin, Caceres, Maxi Pereira, Rodriguez, Arevalo Rios, Gonzalez/Gargano dk83, Forlan, Suarez na Cavani.
Furaha: Brazil wametinfa Fainali kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Uruguay
Shujaa: Paulinho akifunga kwa kichwa bao la ushindi dakika ya 86
La kwanza: Fred akiifungia Brazil dakika nne ya kabla mapumziko
Fred na Neymar wakishangilia mbele ya mashabiki Belo Horizonte
La kusawazisha: Edinson Cavani aliisawazishia Uruguay mapema kipindi cha pili
Kudadadeeki: Cavani alivyofunga
Jitu Kali: Shabiki la Brazil likimsapoto Hulk
No comments:
Post a Comment