Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe amewashauri watu walioko mikoani kusitisha safari za kuja Dar es Salaam wakati wa ziara ya Rais wa Marekani, Barrack Obama kutokana na wingi wa wageni katika jiji hilo.
Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe amewashauri watu walioko mikoani kusitisha safari za kuja Dar es Salaam wakati wa ziara ya Rais wa Marekani, Barrack Obama kutokana na wingi wa wageni katika jiji hilo.
Ugeni huo pamoja na ule wa viongozi kumi na moja
kutoka nchi mbalimbali duniani watakaohudhuria mkutano wa kimataifa wa
Smart Partnership utakaofunguliwa kesho na Rais Jakaya
Kikwete kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, umesababisha kuimarishwa kwa ulinzi katika maeneo mbalimbali hasa katika hoteli za kitalii ambazo zimeanza utaratibu wa upekuzi kwa wageni wake.
Kikwete kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, umesababisha kuimarishwa kwa ulinzi katika maeneo mbalimbali hasa katika hoteli za kitalii ambazo zimeanza utaratibu wa upekuzi kwa wageni wake.
Akizungumza na katika mahojiano na Redio ya Clouds jana, Membe alisema jiji limefurika kwa
“Hoteli na nyumba za wageni zimefurika wageni na
magari mengi yamekodiwa. Kwa ujumla, huduma za kijamii zitakuwa shida,”
alisema.
Rais Obama na mkewe Michelle watawasili nchini
Jumatatu na tayari wapambe na maofisa usalama kutokana Marekani wameanza
kuwasili. Mbali ya ujio huo, wake wa marais kutoka nchi 14 za Afrika
watakaokutana na Laura Bush, mke wa Rais wa zamani wa Marekani, George
Bush. Pia Michelle atahudhuria mkutano huo utakaofanyika Jumanne na
Jumatano ijayo.
“Jiji la Dar es Salaam litakuwa na mambo mengi kwa hiyo wale wenye kuja kutaka kustarehe wafute safari zao,” alisema na kuongeza: “Kama kuna watu ambao hawapo Dar es Salaam na hawana sababu za kuja mjini waache tu mpaka wageni watakapoondoka kwa sababu jiji la litakuwa limejaa na baadhi ya barabara zitachukuliwa zitumike na wageni hao.”
Alisema katika kipindi cha siku tano zijazo, baadhi ya barabara za Jiji la Dar es Salaam zitakuwa na shughuli nyingi na nyingine zitalazimika kufungwa. Barabara itakayofungwa ni pamoja na ile ya Mwai Kibaki na ile ya Bagamoyo itakuwa na shughuli nyingi pia wakati Michelle atakapokwenda Jumba la Makumbusho, Jumanne ijayo.
Wasafiri wa mikoani
Wasafiri wa mikoani wataathirika zaidi Jumanne
ijayo wakati Rais Obama atakapokwenda kutembelea mitambo ya kufua umeme
ya Kampuni ya Symbion Ubungo.
Kituo hicho kipo Barabara ya Morogoro, ambayo ndiyo inayotumiwa na magari yanayoingia na kutoka mikoani.
Rais Obama atakwenda katika kituo hicho yapata saa
4.00 asubuhi na kwa kiasi kikubwa itaathiri magari ya usafirishaji wa
mizigo na abiria yatakayokuwa yanatoka na kuingia Dar es Salaam kabla na
wakati huo.
Wengine watakaoathirika ni wakazi wa Kimara, Mbezi, Kibamba hadi
Kiluvya. Athari nyingine ya usafiri itakuwa katikati ya jiji ambako
Obama na msafara watakuwa na shughuli nyingi na hasa ile ya ufunguzi wa
barabara karibu na Ikulu na kukutana na wafanyabiashara kwenye Hoteli ya
Hyatt Regency, Jumatatu ijayo.
Watumiaji wengine wa barabara watakaopata shida ni
wale wa Barabara ya Bagamoyo hasa pale Rais Obama na mkewe
watakapokwenda kuweka mashada ya maua kwenye ubalozi wa zamani wa
Marekani uliopuliwa na mabomu mwaka 1998.
Ulinzi hoteli za kitalii
Mashushushu wa ndani na nje ya nchi wamezingira
kwenye hoteli kubwa za Dar es Salaam na walionekana katika baadhi ya
hoteli hizo, wakiwatumia mbwa maalumu kufanya ukaguzi wa chumba hadi
chumba.
Tofauti na utaratibu uliozoeleka, baadhi ya hoteli
zenye hadhi ya nyota tano zimeanza kutumia mitambo maalumu ya kompyuta
kuwafanyia ukaguzi wageni wote wanaoingia.
Wamchongea JK
Mtandao wa Kutetea Waandishi wa Habari Duniani
(CPJ), umemwandikia barua Rais Obama ukimtaka kujadiliana kwa kina na
mwenyeji wake Rais Kikwete wakati wa ziara yake nchini kuhusiana na
vitendo vya kuuawa na kuteswa kwa waandishi wa habari wa Tanzania.
Katika barua hiyo iliyosainiwa na Mtendaji Mkuu wa
CPJ, Joel Simon na nakala yake kusambazwa kwa viongozi mbalimbali
akiwemo Rais Kikwete mwenyewe, mtandao huo ulitolea mfano wa kuuawa kwa
Mwandishi wa Channel 10, Daudi Mwangozi na Issa Ngumba wa Redio Kwizera.
Pia kupigwa na kuteswa kwa Mhariri Mtendaji wa Habari Corporation,
Absalom Kibanda.
Marais waja Smart Partnership
Akizungumzia mkutano wa Smart Partnership utakaoanza kesho,
Membe alisema utajadili jinsi ya kutumia sayansi na teknolojia kukuza
uchumi.
Viongozi watakaohudhuria mkutano huo ni Waziri
Mkuu wa Malayasia, Najib Razak, Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, Uhuru
Kenyetta (Kenya), Boni Yayi (Benin), Ali Omar Bongo (Gabon), Ikililou
Dhoinine (Comoro), Faure Gnassingbe (Togo), Ernest Koroma (Sierra
Leone), Blaise Compaore (Burkina Fasso), Mahinda Rajapaska (Sri Lanka)
na Mfalme wa Swaziland, Mswati II, ambaye aliwasili jana
No comments:
Post a Comment