Muheza.
Serikali imepiga marufuku uuzaji mahindi mabichi maeneo yote wilayani hapa.
Serikali imepiga marufuku uuzaji mahindi mabichi maeneo yote wilayani hapa.
Agizo hilo lilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Subira Mgalu, kutokana na kukithiri kwa uuzaji mahindi mabichi.
Mgalu alisema ni marufuku kuuza mahindi mabichi hasa yanayochomwa kwenye vijiwe mjini na vijijini, kuchemsha na kusafirisha.
Alisema hiyo ni amri halali na kwamba, mtu yeyote atakayepatikana na kosa hilo atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Mgalu alisema kutokana na kasi ya uuzaji mahindi, kuna hatari ya kusababisha baa la njaa katika wilaya hiyo. Alisema inatakiwa wananchi kujenga tabia ya kutunza chakula, badala ya kuelekeza fikira kwenye uuzaji baadaye wanaanza kuomba chakula cha msaada.
“Wananchi watunze chakula kwani kuuza hakuwezi kumaliza matatizo yenu... hayataisha kwa kuuza mahindi mabichi,” alisema.
No comments:
Post a Comment