Stori: Gladness Mallya na Hamida Hassan
HAYA ni mateso 100%! Dereva mmoja wa boda boda mkazi wa Kimara King’ongo jijini Dar es Salamaa anayejulikana kwa jina la Joseph Nyunza, yupo katika mateso makali yaliyosababishwa na Sangoma aliyeng’oa vyuma alivyowekewa hospitalini na kusababisha mguu wake kuoza.

Akizungumza
na gazeti hili akiwa hoi kitandani nyumbani kwa shangazi yake, Joseph
alisema awali alikuwa dereva wa pikipiki lakini Julai mwaka huu, alipata
ajali maeneo ya Kimara Suka jijini Dar es Salaam baada ya kugongwa na
gari lililohama njia na kumvunja mguu wake wa kulia.
Baada ya kupata
ajali hiyo, alikimbizwa Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako alipokelewa
na kupelekwa katika kitengo cha mifupa (Moi) ambako baada ya kufanyiwa
vipimo, iligundulika kuwa mfupa mkubwa wa mguu wake ulivunjika, hivyo
kuwekewa vyuma ‘antena’ ili uweze kuunga. Aliruhusiwa kurudi nyumbani
huku akitakiwa kurejea tena hospitalini kwa ajili ya upasuaji.
Baada
ya kurejea nyumbani na kukaa wiki kadhaa huku akitembelea magongo,
alikosa fedha za kurudi hospitalini kwa ajili ya upasuaji ndipo
alipojitokeza mganga wa jadi aliyemtaja kwa jina la Mama Sura aliyeahidi
kumponya kidonda hicho.
Mganga huyo alimpaka dawa zake kwa siku
kadhaa lakini hakuona nafuu yoyote. Kuona hivyo, Sangoma huyo alishauri
kuondolewa kwa vyuma hivyo vya kitaalamu vingeuwezesha mguu huo kuunga
vizuri.
“Kweli, siku iliyofuata mganga wangu alikuja na mtu mwingine,
akanitoa vyuma bila ganzi, niliumia sana lakini nilivumilia kwa sababu
alinihakikishia ningepona.
“Kadiri siku zinavyozidi kwenda ndiyo mguu unazidi kutoa wadudu wa chooni, jamani ninaomba mnisaidie Watanzania wenzangu, ninateseka sana mimi,” alisema Joseph.
Alisema baada ya kutolewa vyuma hivyo, aliendelea kupakwa dawa hizo za kienyeji kiasi kwamba hadi sasa mguu umeoza na unatoa funza huku kijana huyo akiwa hawezi hata kunyanyuka kitandani.
MGANGA ANASEMAJE?
Baada ya mapaparazi wetu kuzungumza na Joseph walimtafuta mganga huyo ambaye pia anaishi maeneo ya King’ong’o, hakuwepo nyumbani lakini alipatikana kwa njia ya simu.
“Mimi sijamkuta na hali hiyo aliyonayo sasa, naamini anaendelea vizuri na atapona kwa sababu nimeshawatibu watu wengi sana wa aina hiyo, mbona sasa hivi ana nafuu, muulizeni mwenyewe atawaambia,” alisema
MWENYEKITI ANENA
Naye Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa King’ong’o, Demetrius Mapesi amekiri kupokea taarifa hizo kwa masikitiko na kuanzisha harambee ya kumsaidia kupitia namba 0654 880707.

CHANZO NI GLP
No comments:
Post a Comment