Makala: Sifael Paul na Mitandao
FLORA Mbasha ni mwimba Injili Bongo mwenye ‘profaili’ kubwa ndani na nje ya Tanzania. Kama ulikuwa hujui, ni mmoja wa mastaa wengi wakubwa wa ‘gospo’ watakaoshusha upako kwenye Tamasha la Matumaini litakalofanyika katika Uwanja wa Taifa, Dar, Julai 7, mwaka huu.
Flora alizaliwa jijini Mwanza mwaka 1983 katika familia ya Dini ya Kikristo. Ni mtoto wa pili kwenye familia ya Henry Mayallah na Caroline Moses Kulola.
Alimpoteza baba yake mwaka 1998. Kwa wakati huo walikuwa wakiishi jijini Arusha, akamwacha Flora na nduguze Benjamin na Dorcus.
Baada ya baba kufariki dunia walirejea Mwanza ambapo walilelewa na babu yao ambaye wengi wanamjua, Askofu Moses Kulola wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God la Mwanza.
“Nimekulia mikononi mwa kanisa tangu nikiwa mdogo. Nawashukuru babu na bibi yangu kwa kunilea tangu nilipompoteza baba yangu. Walinifundisha kwa kipindi chote hadi nilipoolewa,” anasema Mbasha katika mahojiano na runinga moja London, Uingereza.
Baadaye mama yao aliolewa na mwanaume mwingine na kujaliwa mabinti wawili, Suzy na Esther. Flora alihitimu masomo ya sekondari katika Shule ya Taqwa, Mwanza mwaka 2000.
NDOA
Agosti 22, 2002, Flora alifunga ndoa na mwimba Injili, Emmanuel Mbasha wakiwa Mwanza na mtoto wao wa kwanza anaitwa Elizabeth. Agosti 22, mwaka huu watatimiza miaka 11 ya ndoa bila ‘kikohozi’ yaani bila migogoro au kuvunjika kama zilivyo baadhi ya ndoa za mastaa wengine Bongo. Wanapendana mno, mahali alipo Flora lazima utamuona Mbasha.
Flora anakiri kuwa mafanikio aliyopata yana mchango mkubwa wa ushirikiano anaopata kutoka kwa mumewe Mbasha.
“Mume wangu amekuwa msaada mkubwa wa mafanikio yangu,” anasema Flora ambaye kwa sasa anaishi na familia yake katika nyumba waliyojenga Tabata, Dar.
Anaendelea: “Ananisapoti (Mbasha) kwa kunipa ushauri sahihi na kuniongoza kuwa hivi nilivyo leo. Tumeandika nyimbo pamoja na kupafomu katika albam zangu zote nilizonazo.
MUZIKI WA GOSPO
Flora alianza muziki wa ‘gospo’ tangu akiwa mdogo akiimba kwaya kanisani. Anasema pamoja na ubunifu binafsi lakini pia alikuwa akiwaiga waimbaji wengine kwenye kwaya kanisani na kwenye mikutano ya Injili. Baadaye alimtamani kuwa kama mwimba Injili wa Afrika Kusini ‘Sauzi’, Rebecca Malope.
“Nilianza kuimba nikiwa mdogo sana. Nilikuwa nikiimba kwenye Kwaya ya Bugando Divine Singers ya Mwanza,” anasema na kuongeza:
“Baadaye, kwa msaada mkubwa wa mume wangu nilifanikiwa kurekodi albamu yangu ya kwanza ya Jipe Moyo Utashinda katika Studio ya Backyard chini ya Prodyuza Hingi.”
NYIMBO ZOTE KALI
Katika albam hiyo utakutana na nyimbo zenye upako kama Maisha Ya Ndoa, Hakuna Tatizo Kuu, Ukimwi, Yu Karibu, Aliteseka, Tunaye Bwana, Majaribu, Ahsante Yesu na Kila Jambo.
Katika albam yake ya pili iliyokwenda kwa jina la Unifiche, utapata utamu wa nyimbo zake kama Tanzania, Nifiche, Faida Gani, Twende Kwa Yesu, Ninalia, Kwa Kupigwa Kwake, Kristo Amezaliwa na Tupendane.
“Namshukuru Mungu kwa albam ya pili, ilinipa Tuzo ya Mwimbaji Bora wa Gospel mwaka 2004. Niliandika wimbo kwa ajili ya nchi yangu, nikaupa jina la Tanzania. Ulinifanya nijulikane zaidi ndani na nje ya Bongo,” anasema.
Mwaka 2008, Flora aliachia albam yake ya tatu iliyoitwa Furaha Yako ikiwa na nyimbo kali 12 kama Furaha Yako, Rudi Nyuma, Adui Yako, Tutamwona, Nibariki, Tufurahie, Mteule Usiogope, Natembea na Yesu, Anaweza, Jerusalemu, Mwanamke na Usife Moyo.
MALENGO
Malengo ya Flora ni kufanya watu wazaliwe upya katika Kristo ndiyo maana nyimbo zake zimejaa mafundisho ya Mungu.
Malengo ya Flora ni kufanya watu wazaliwe upya katika Kristo ndiyo maana nyimbo zake zimejaa mafundisho ya Mungu.
Flora
amezunguka mikoa mingi Bongo na nje ya nchi kama Marekani, Uingereza,
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kwingineko. Kote alikopita
alipokelewa kwa kishindo na akatoa mafundisho ya Mungu kwa njia ya
nyimbo.
“Nimefanikiwa kushika mioyo ya watu wengi wanaopenda muziki
wa Injili hasa wale wasiokuwa na uwezo wa kifedha kwa ajili ya kulipia
kuingia kwenye matamasha,” anasema Flora na kuongeza:
“Ndoto yangu ni kumtumikia Mungu katika maisha yangu hadi atakaponiita. Watu lazima wabadilike, waachane na madawa ya kulevya, pombe na umalaya kisha wamrudie Mungu.
“Moyo wangu unauma sana ninapowaona vijana wakitenda dhambi.”
UTUKUFU UTASHUKA!
Flora anayependa kuchati na marafiki ataangusha shangwe za upako kupitia nyimbo zake nyingi nilizokudonolea kidogo hapo juu na nyingine nyingi mpya katika tamasha hilo la Matumani akiwa na Upendo Nkone, Martha Mwaipaja, Edson Masabwite, Ambwene Mwasongwe, Glorious Worship Team, Emmanuel Mgaya ‘Masanja’, Enock Jackson, The Voice na Jesca.
Kutoka Kenya atachuana na Anastazia Mukabwa, Solomon Mukubwa, Sara K na 24 Elders.
“Ndoto yangu ni kumtumikia Mungu katika maisha yangu hadi atakaponiita. Watu lazima wabadilike, waachane na madawa ya kulevya, pombe na umalaya kisha wamrudie Mungu.
“Moyo wangu unauma sana ninapowaona vijana wakitenda dhambi.”
UTUKUFU UTASHUKA!
Flora anayependa kuchati na marafiki ataangusha shangwe za upako kupitia nyimbo zake nyingi nilizokudonolea kidogo hapo juu na nyingine nyingi mpya katika tamasha hilo la Matumani akiwa na Upendo Nkone, Martha Mwaipaja, Edson Masabwite, Ambwene Mwasongwe, Glorious Worship Team, Emmanuel Mgaya ‘Masanja’, Enock Jackson, The Voice na Jesca.
Kutoka Kenya atachuana na Anastazia Mukabwa, Solomon Mukubwa, Sara K na 24 Elders.
CREDIT:GLP
No comments:
Post a Comment