Jacqueline Wolper ‘Wolper Gambe’ amedai hawapendi wanaume wenye
fedha kwani wengi wao ni waume za watu na si rahisi kuonyesha mapenzi
yao ya dhati kwake, pia hawezi kutembea nao hadharani kwa kuhofia ndoa
zao.
“Unajua unapokuwa na mtu mwenye fedha zake halafu mtu mzima hivi unakosa penzi la kweli. Mapenzi yenu yatakuwa ya chumbani tu,” alisema.
“Hamtaweza kutembea pamoja, lakini ukiwa na kijana ambaye ni rafiki hana pesa na wewe una kazi lazima akuonyeshe jinsi mapenzi yalivyo kwa kukuweka karibu kimahaba na wewe ukafaidi penzi kutoka kwake.
“Wengi wenye fedha zao kuna wakati wananiona nina dharau, lakini mimi ni binadamu nahitaji haki yangu kama mwanamke, ninahitaji kuwa na mtu anayenijali na kuwa karibu na mimi.
“Kuna watu wanaamini fedha zao ndio kila kitu, kiukweli kwangu siyo hivyo ukileta mapenzi hayo lazima unione nina dharau.”
Anasema wengine huwanyooshea vidole wasanii
maarufu kama yeye kwa kuwaona kama vile ni malaya, lakini wanasahau kuwa
nao ni binadamu.
“Kila binadamu anapenda na kupendwa,” alisema.
No comments:
Post a Comment