Lagos, nigeria
KUNA watu wamekuwa wakihangaika usiku na mchana kusaka umaarufu.
KUNA watu wamekuwa wakihangaika usiku na mchana kusaka umaarufu.
Kwa wale walio chini wamekuwa wakifanya mambo mengi hata yale ya kuhatarisha maisha ilimradi kuhakikisha malengo yao yanatimia.
Lakini kwa wale ambao ni maarufu, baadhi yao wamekuwa wakijisikia vibaya na wakati mwingine kujuta kuwa maarufu kutokana na kuchukuliwa tofauti na jamii zao, Emeka Ike ni mmoja wao.
Anasema: “Kusema ukweli wakati mwingine najuta kuwa mwigizaji maarufu, sina usiri, mara nyingi huwa ni karaha maana watu huchukulia uigizaji kama maisha halisi ya wasanii. Hivyo kuleta shida.
Wanasahau kuwa uigizaji ni kazi kama kazi nyingine.
“Kutokana na ukweli huo tumekuwa tukiitwa majina mabaya na hata kudhaniwa visivyo na wakati mwingine kubezwa mitaani.”
No comments:
Post a Comment