Mjasiriamali
mchapakazi na Mbunge Kijana nchini Tanzania, Mohammed Dewji (MO)
ametajwa katika jarida la Kimataifa la mabilionea duniani katika Nyanja
za biashara (Forbes Africa Magazine) kama mjasirimali mwenye umri mdogo
mwenye mafanikio ya kuigwa hapa Afrika na duniani kwa ujumla taarifa la
Jarida hilo limeeleza.
Kwa
mujibu wa taarifa hizo toka kwa Jarida hilo la Forbes African Magazine
linasema amekuwa Mtanzania wa Kwanza kupata kuhojiwa na (Forbes
Magazine) mafaniko, changamoto na matatizo kadhaa kwenye uwanja wa
biashara kwenye ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati.
Mo
akihojiwa na Jarida hilo alisema toka kwenye masaa mia moja kwa wiki na
kutengeneza faida ya Millioni 85 dola za kimarekani! Ni mafanikio
makubwa katika biashara Afrika.
Anasema ni safari ya takribani miaka 12 ya ushindani wa kibiashara ndani ya mipaka ya Tanzania na Afrika kwa ujumla.
"Nani
anaweza kufikiri kwamba tunaweza kubadilisha biashara yetu toka Millioni
30 za kimarekani hadi dola Billioni 1.1 ndani ya miaka 12 tu,'
alinukuliwa akisema.
No comments:
Post a Comment