MKURUGENZI wa Kampuni
ya Principal Company Limited, Godfrey Mosha ameieleleza Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam jinsi Benki ya Akiba Commercial Tawi
la Ubungo ilivyoidhinisha malipo ya fedha kwa mtu mwingine kutoka
katika akaunti yake ndani ya benki hiyo, bila yeye kuwa na taarifa wala
kuridhia.
Katika kesi hiyo ya madai ya uzembe iliyofunguliwa na Mosha dhidi ya Benki ya Akiba, inayosikilizwa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Warialwande Lema, Mosha anaomba Benki hiyo imlipe Sh.milioni 46.8 , zilizolipwa kwa mtu asiyemfahamu kwa kutumia hundi nne tofauti na kwa tarehe tofautitofauti ambazo alidai hundi hizo zimeghushiwa.
Akiongozwa na wakili wake Michael Ngaro kutoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Lema, Mosha ambaye ni mlalamikaji katika kesi hiyo, alidai kuwa aligundua hamisho hilo la kiasi hicho cha fedha katika akaunti ya

kampuni yake Na. 0400438671, Novemba 15, 2011, alipochukua taarifa ya kibenki (Bank Statement).Mosha
alidai kuwa baada ya kubaini hamisho hilo , alikwenda makao makuu ya
benki hiyo ambako alimuona Meneja wa Fedha, Vicent Antony na kumwalifu
kuhusu tukio hilo wakati yeye hajawahi kuidhinisha hamisho hilo.
“Vicent aliniambia kuwa siyo transfer (hamisho) bali ni malipo yaliyofanyika kwa kutumia cheque. Aliniambia namba za hundi hizo na ikaonekana kuwa zililipwa kwa Rafael John Mkwabi, mwenye namba ya akaunti 11000787541.”, alidai Mosha na kuongeza: “Binafsi huyo John sijawahi kumwandikia hundi wakati wowote ule , wala sijawahi kufanya naye biashara, sijawahi kukutanana naye, wala simfahamu kabisa.”
Mosha alidai kuwa hundi hizo zilikuwa zimesainiwa na Vicent na Meneja Mkuu, Salehe Ramadhani, huku akidai kuwa saini inayoonekana katika hundi hizo si yake.
Alizitaja hundi hizo kuwa ni hundi namba 083722, ya Sh11.6 milioni iliyolipwa Novemba 11, 2011 na hundi namba 083723, ya Sh 9 milioni, pia iliyolipwa tarehe hiyo.Hundi nyingine ina namba 083724 , ya Sh milioni 14.4 iliyolipwa Desemba 2011, na hundi namba 083725, ya Sh.milioni 11.8 iliyolipwa Desemba 3, 2011.
Mosha kupitia wakili wake Ngaro alizitoa hundi hizo na nyaraka nyingine mbalimbali na kuomba zipokelewe kama vielelezo.Na baada ya kumaliza kutoa ushahidi wake, wakili , Ngalo alifunga ushahidi na hakimu Lema aliarisha kesi hiyo hadi Julai 8 mwaka huu, iyakapokuja kwaajili ya mdaiwa ambaye ni benki ya Akiba inayotetewa na wakili wa kujitegemea Karoli Tarimo waanze kujitetea.

via Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment