MWILI wa aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya, marehemu
Albert Mangwea ‘Ngwair’ sasa unatarajiwa kuwasili nchini kesho badala ya
leo kama ilivyotaarifiwa awali.
Kwa mujibu wa taarifa ya kamati ya mipango ya mazishi ya msanii huyo
iliyotolewa jana inayoongozwa na Kaka wa marehemu, Kenneth Mangwea,
mwili huo utawasili Jumapili majira ya saa 8, mchana na kisha kufuata
taratibu zingine.
“Mwili utafika nchini siku ya Jumapili majira ya saa nane mchana na
sio Jumamosi (leo), kama ilivyotaarifiwa hapo awali,” ilieleza taarifa
hiyo.
Sababu za mabadiliko hayo, imeelezwa ni kutokana na Watanzania waishio
Afrika Kusini, kuomba kutoa heshima za mwisho, Jumapili.
Kwa hatua hiyo, kamati ilibainisha kuwa kwa wakazi wa Dar es Salaam na
maeneo ya jirani, watapata nafasi ya kuuaga mwili Jumatatu majira ya
saa 2 asubuhi hadi 6 mchana na baada ya hapo, wataelekea Morogoro kwa
ajili ya mazishi, Jumanne.
Aidha, kamati iliomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza, huku
ikiomba wadau kuendelea kuwaombea kufanikisha salama shughuli hizo za
mazishi.
No comments:
Post a Comment