EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, June 27, 2013

NI wazi sasa, inaonekana ulimi umemponza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, baada ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kuendesha kazi ya kukusanya saini za watu mbalimbali ili kumwajibisha.

Kituo hicho kimesema hadi jana, kilikuwa kimekusanya saini 1,000 za watu mbalimbali ambazo zinamtaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kufuta kauli yake aliyoitoa bungeni wiki iliyopita.

Wiki iliyopita, Pinda alitoa baraka zote kwa Jeshi la Polisi nchini kutumia nguvu dhidi ya watu wote wanaovunja amani na utulivu, wakati akijibu maswali ya papo kwa papo mjini Dodoma.

Katika kauli yake, alivitaka vyombo vya ulinzi, hasa Jeshi la Polisi kuwapiga watu watakaokaidi au kupinga amri halali zinazotolewa na vyombo hivyo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa LHRC, Dk. Helen Kijo Bisimba, alisema kamwe hawakubaliani na kauli ya Pinda, kwa sababu haifuati haki za binadamu.

Alisema ni aibu kauli hiyo kutolewa na kiongozi wa juu serikalini, kwani inaonyesha wazi imevunja Katiba, sheria na misingi ya haki za binadamu.

Alisema Pinda, hatafuta kauli yake au kuomba radhi Watanzania, wao kama kituo watajua njia gani ya kufanya ili kulinda maisha ya Watanzania.

Alisema katika saini hizo, kituo chake kimezipokea kutoka maeneo mbalimbali, yakiwamo ya Kinondoni (Dar es Salaam), Chato, Biharamulo (Kagera), Temeke (Dar es Salaam).

Alisema mpaka jana, wananchi wengi wanaendelea kutuma saini zao kwa njia ya mtandao.
“Tunamtaka Waziri Mkuu Pinda, afute kauli yake aliyoitoa bungeni kubariki polisi kupiga raia katika mkutano huu wa Bunge la Bajeti au aombe radhi kwa Watanzania kwa kile alichokisema bungeni.

“Tunapenda kumkumbusha, utawala wa sheria unajumuisha serikali, vyombo vya utekelezaji na ulinzi pamoja na wananchi kuheshimu sheria na si kuvunja sheria…tamko hili limetoa mwanya mkubwa wa nguvu kwa vyombo vya usimamizi wa sheria kuvunja haki za raia.

“Hali hii ni ya kushtusha kwenye nchi yenye utulivu na amani na kama tunavyopenda kusema kisiwa cha amani, kiongozi huyu wa ngazi za juu anatoa tamko linaloashiria kutoa ruksa kwa Jeshi la Polisi kuvunja tena sheria, tunasema hatukubaliani nalo kamwe,” alisema Dk Bisimba.

Alisema katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na matukio mengi ya ukiukwaji wa haki za binadamu, hasa yale yanayotokana na vyombo vya dola na Jeshi la Polisi, kwa kupiga na kuua watu kwa risasi za moto.

Waziri Pinda alitoa kauli hiyo bungeni, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu (CCM), aliyetaka kujua hatua zinazochukuliwa na serikali kutokana na matukio ya vurugu mara kwa mara nchini, hususani katika mikoa ya Mtwara na Arusha.

Katika swali hilo, Pinda alijibu: “Na mimi nasema wanaokaidi amri halali ya Jeshi la Polisi muwapige tu, kwa sababu hakuna namna nyingine ya kupambana na wakaidi zaidi ya kuwapiga”.

Kauli hiyo, pia ilipingwa vikali na Jaji mstaafu, Mark Bomani, ambaye alisema kutumia vyombo vya dola kudhibiti au kupiga watu kama ilivyoamuliwa na Pinda, haikubaliki.
Via Tanzania Daima

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate