WAKAZI wawili wa Dar es Salaam, wamekamatwa na dawa za kulevya
wakijiandaa kuzisafirisha nje ya nchi. Akizungumza Dar es Salaam jana,
Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya cha Jeshi la Polisi,
Godfrey Nzowa, alisema mkazi wa Mbezi Beach, Saada Kilongo (26),
amekamatwa kwa kukutwa na kilogramu 11 za dawa za kulevya aina ya
Ephedrine.
Alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa alfajiri ya Juni 23, 2013 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere (JNIA).
“Mtuhumiwa alikutwa na passport yenye No. AB527692, iliyotolewa Juni 27, 2012, Dar es Salaam, alikuwa akizisafirisha dawa hizo kwenda Afrika Kusini zikiwa zimefichwa ndani ya begi lake, ambapo awali alidai kuwa ni sukari lakini tulivyozipeleka kwa Mkemia wetu, ikabainika kuwa ni dawa za kulevya.
“Siku hizi wasafirishaji wa dawa hizi wamekuwa ni wajanja, kwa kuwa kama ukiona jinsi alivyohifadhi katika mifuko utadhani kwamba ni sukari kweli na ni vigumu kugundua kwa kuwa hata harufu wameweka mfano wa kahawa,” alisema Nzowa.
Alisema kwa mujibu wa
maelezo ya mtuhumiwa huyo alidai dawa hizo alizitoa nchini India na kuja
nazo Tanzania kwa lengo la kuzisafirisha kiurahisi.Alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa alfajiri ya Juni 23, 2013 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere (JNIA).
“Mtuhumiwa alikutwa na passport yenye No. AB527692, iliyotolewa Juni 27, 2012, Dar es Salaam, alikuwa akizisafirisha dawa hizo kwenda Afrika Kusini zikiwa zimefichwa ndani ya begi lake, ambapo awali alidai kuwa ni sukari lakini tulivyozipeleka kwa Mkemia wetu, ikabainika kuwa ni dawa za kulevya.
“Siku hizi wasafirishaji wa dawa hizi wamekuwa ni wajanja, kwa kuwa kama ukiona jinsi alivyohifadhi katika mifuko utadhani kwamba ni sukari kweli na ni vigumu kugundua kwa kuwa hata harufu wameweka mfano wa kahawa,” alisema Nzowa.
Katika hatua nyingine, alisema Juni 26, 2013 eneo la JNIA, walimkamata mtuhumiwa mwingine mkazi wa Bungoni Ilala, Haji Mintanga (30), kwa kosa la kukutwa na kilogramu mbili za dawa za kulevya aina ya heroin alizokuwa akizisafirisha kwenda Ugiriki kupitia Uturuki.
“Mintanga tulimkamata saa mbili asubuhi akiwa anajiandaa kusafirisha dawa hizo ambazo alikuwa amezificha ndani ya begi lake,” alisema Nzowa.
Kutokana na kuongezeka kwa watuhumiwa wanaokamatwa na dawa hizo za kulevya hapa nchini, alisema hiyo ni kati ya changamoto wanazokumbana nazo, kutokana na watu hao kuwa na mtandao mkubwa wa watu wanaojihusisha na vitendo hivyo.
“Kwa yeyote anayejihusisha na vitendo hivi, anatakiwa aachane navyo mara moja kwa kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi yao na tunawaomba wananchi kuendelea kutupa taarifa wanaojihusisha na biashara hii haramu tuweze kuwadhibiti,” alisema Nzowa.
No comments:
Post a Comment