SEND OFF ya ua zuri kwenye soko la filamu Bongo, Flora Mvungi iliyofanyika Jumanne iliyopita Msasani Beach, Mikocheni jijini Dar imepigwa umbea kuwa ni bosheni kwani hata ndoa yake na Hamis Ramadhan ‘H. Baba’ haitadumu kutokana na tabia ya wasanii kutodumu kwenye ndoa.

“Yaani hiyo ndoa mimi nawaambia nawapa mwaka mmoja tu mtaniambia kama
kutakuwa na ndoa tena, wasanii ni wasanii tu hata iweje. Tatizo lao
wanaleta maisha ya kuigiza hadi kwenye filamu.
“Tazama ndoa ya Uwoya ilivyokuwa ya gharama, mbwembwe nyingi lakini
mwisho imekuja kuparanganyika huku kila mmoja akimtafuta mwenzake
uchawi,” alisema msanii huyo ambaye anaonesha ‘kuwajua’ vizuri wanandoa
hao.
Siku ya send off, Flora alipotinga ukumbini na kubadilisha mavazi
zaidi ya matatu, ilidaiwa kuwa ni ufahari na mara nyingi huwa ndoa za
namna hiyo kwa mujibu wa msanii huyo hazidumu.
“Ni mbwembwe tu
zisizokuwa na msingi wowote, Flora na H. Baba tunawajua vizuri, kama
hamuamini subirini mtaona, ikizidi mwaka mmoja ni bahati,” alisema.
Hata hivyo, Flora baada ya kumaliza sherehe hiyo alidai kuwa anamuomba Mungu ndoa yao idumu milele na milele ili kuwakata vilimi wambeya wote wasioitakia mema ndoa yao.
Hata hivyo, Flora baada ya kumaliza sherehe hiyo alidai kuwa anamuomba Mungu ndoa yao idumu milele na milele ili kuwakata vilimi wambeya wote wasioitakia mema ndoa yao.
“Tunamuomba Mungu ndoa yetu idumu vizazi
na vizazi na hao wanaochongachonga kila kukicha wabaki midomo wazi sisi
maisha yanaendelea,” alisema Flora.
Sherehe hiyo ya send off ilihudhuriwa na mastaa kadhaa wa Bongo Movies akiwemo Jacqueline Wolper, Mahsein Awadh ‘Dk Cheni’, Isabela Mpanda na Luteni Kalama.
Sherehe hiyo ya send off ilihudhuriwa na mastaa kadhaa wa Bongo Movies akiwemo Jacqueline Wolper, Mahsein Awadh ‘Dk Cheni’, Isabela Mpanda na Luteni Kalama.
No comments:
Post a Comment