MSANII wa filamu za Kibongo,
Shamsa Ford amesema kuwa anajuta kukimbilia kuishi na mwanaume kabla ya
kufunga ndoa hali inayomfanya aogope kuolewa kwa kuhofia kushindwa
maisha hayo.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Shamsa alisema amekuwa akitamani
kuishi bila ya mwanaume tofauti na anavyoishi na mchumba wake wa muda
mrefu, Dick.
“Yaani sikufichi kabisa, najuta kwa nini nilikimbilia kuishi na mwanaume kabla ya kufunga ndoa maana hivi sasa nimeshachoka na natamani kuishi peke yangu,” alisema.
“Yaani sikufichi kabisa, najuta kwa nini nilikimbilia kuishi na mwanaume kabla ya kufunga ndoa maana hivi sasa nimeshachoka na natamani kuishi peke yangu,” alisema.
Kutokana na hali hiyo, msanii
huyo amesema ndiyo maana amekuwa akikwepa kufunga ndoa na mwanaume huyo
aliyezaa naye mtoto mmoja kutokana na kuchoka kuishi pamoja kwa kuhofia
misukosuko ya ndoa.
“Naogopa hata kufunga ndoa kwa kuwa
nimeshachoka kuishi na mwanaume, sasa nikifunga ndoa naona kama vile
itanishinda mapema,” alisema Shamsa.
Via GLP
No comments:
Post a Comment