Mmoja
wa washiriki wa shindano la Bibi Bomba awamu ya pili Bi.Anna Nicholaus
akikabidhiwa fulana yenye jina lake na mmoja wa Waratibu wa shindano
hilo,AJ Jonathan,wakati wa utambulisho rasmi wa washiriki hao mapema
jana jioni mbele ya Wanahabari (hawapo pichani), uliofanyika kwenye
ukumbi wa alliance française,jijini Dar.Aidha pia washiriki hao wapatao
ishirini walipata nafasi ya kusaini mikataba yao na pia kuelezwa
utaratibu mzima wa mchakato wa Bibi Bomba 2013.
Bi.Anna
Nicholaus akivalishwa fulana yake ya ushiriki kutoka kwa mmoja wa
waratibu wa shindano hilo lenye msisimko mkubwa,Asmah Makau.
Mshiriki
mwingine wa shindano la Bibi Bomba, Bi.Tabitha Tungaraja akishukuru
Mungu mara baada ya jina lake kutajwa na kuingia kwenye ushiriki wa
shindano hilo, mbele ya baadhi ya waratibu wa shindano zima.
Pichani
wa pili kushoto ni Meneja wa Clouds TV ambao ndio warushaji wa shindano
la Bibi Bomba season 2,Bwa.Lee Ndayisaba akifafanua jambo mbele ya
washiriki wa shindano hilo na wanahabari (hawapo pichani) kuhusiana
uendeshaji na mchakato mzima wa shindano hilo ambalo limekuwa na
msisimko mkubwa kwa watazamaji.Shoto ni mmoja wa waratibu wa shindano
hilo Babuu wa Kitaa (Clouds TV),tatu shoto ni wawakilishi wa shirika la
USAID,Bi.Naomi Kaspar pamoja na Dkt.May Bukuku, ambao wametoa mchango
mkubwa kufanikisha maandalizi ya shindano hilo.
Baadhi
ya washiriki wa shindano la Bibi Bomba awamu ya pili 2013 wakiwa ndani
ya ukumbi wa alliance française wakisiliza mchakato mzima wa utaratibu
wa shindano hilo.
Baadhi ya Mabibi Bomba wakifurahi jambo.
Shindano
hilo lilianza mchakato wake wa usaili katika viwanja vya Leaders Club,
ambapo Mabibi zaidi ya 60 walijitokeza aidha kati yao waliingia katika
mchujo wa awali na kupatikana Mabibi 20 ambao wameendelea kupigiwa kura
hadi hii leo.
Shindano la Bibi Bomba season 2 limezinduliwa rasmi hapo jana katika ukumbi wa Alliance Française, ambapo bibi 20 wanaingia rasmi katika kinyanganyiro cha kumtafuta bibi Bomba kwa mwaka 2013.
"siku zote panapokuwa na watu wengi lazima vituko, kero ama ubabe lazima vinanafasi ya kujitokeza ili kutimiza ule msemo wa kiswahili unaosema “penye wengi kuna mengi” ..tunatarajia msisimko wa aina yake katika mashindano haya kwa mwaka huu.
tofauti pia na mwaka jana ambapo shindano hili lilidumu kwa mwezi mmoja,na mwaka huu Bibi bomba itachukua takriban miezi 3.Mengi mtayapata wakati kipindi kikiwa kinaruka kuanzia saa mbili na nusu usiku",alimaliza kusema Lee wa Clouds TV ,kituo ambacho kitakuwa kikirusha shindano hilo.
No comments:
Post a Comment