
Baadhi ya websites zimeandika kuwa Brother Dully Sykes hakuenda kuupokea wala kuuaga mwili wa marehemu Albert “Ngwair” Mangwea, na badala yake alikuwa akila bata na mpenzi wake.
Ukweli ni kwamba siku moja baada ya kifo cha marehem Ngwea, Dully alienda Mwanza, na alikaa huko kwa siku mbili.
Alipokua anarudi kutoka Mwanza, kwa kuwa alikuwa akiendesha gari mwenyewe, Dully aliamua kubaki Morogoro tangu Jumatatu kuusubiri mwili wa Ngwea. Hivyo Dully hakuwa akifanya starehe, bali alikua yupo na Afande Sele na wananchi kibao maeneo ya nane nane, wakisubiri kuusindikiza mwili wa marehemu kutoka maeneo hayo – Diamond
No comments:
Post a Comment