BENDI za Msondo Ngoma, Mlimani Park Ochestra ‘Sikinde Ngoma ya Ukaye’ na
Jahazi Modern Taarabu, zinatarajia kunogesha kwenye Tamasha la Usiku wa
Matumaini litakalofanyika Julai 7, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam.

Mratibu wa Tamasha hilo ambalo kwa mwaka huu litafanyika kwa mara ya
pili, Abdallah Mrisho ‘Abby Cool’, alisema tayari makundi hayo yameahidi
kutoa burudani kali kwa mashabiki watakaojitokeza siku hiyo ambayo
itakuwa ni Sikukuu ya Sabasaba.
Tamasha hilo lenye kauli mbiu ya
Tuna Dini na Itikadi Tofauti Lakini Sisi Sote ni Wamoja, lina lengo la
kuendeleza amani huku sehemu ya mapato yake ikitarajiwa kuchangia mfuko
wa elimu kupitia kwa Mamlaka ya Elimu Tanzania (Tea).
Viingilio vya tamasha hilo vitakuwa kama ifuatavyo: VIP shilingi 20,000, viti vya bluu 10,000 na mzunguko 5,000.
Mwaka jana tamasha hilo lilifana sana, lakini mwaka huu Abby Cool
amesema mambo yatakuwa bomba zaidi, kwani maandalizi yanayofanyika ni ya
viwango vya kimataifa. Tazama baadhi ya vipengele:
No comments:
Post a Comment