



SIMANZI, vilio na majonzi
vilitawala nyumbani kwa Mama Mzazi wa marehemu Jaffari Ally, Bi. Rehema
Tuwa, Tandale jijini Dar. Marehemu Jaffari ambaye alikuwa ni mume wa
Malkia wa Mipasho nchini, Khadija Kopa amefariki dunia usiku wa kuamkia
leo katika hospitali ya Jeshi ya Lugalo. Marehemu Jaffari alikuwa Diwani
wa kata ya Magomeni wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani wakati mama yake
mzazi ni Mwenyekiti wa UWT Tandale. Mungu ailaze roho ya marehemu
Jaffari Ally mahali pema peponi. AMEN!
(PICHA NA RICHARD BUKOS/GPL)
No comments:
Post a Comment