WATU
wawili wamekamatwa jijini Dar es Salaam wakituhumiwa kufanya wizi kwa
njia ya mtandao katika Benki ya Azania kwa kuhamisha akaunti, kubadili
picha na saini na kuweka picha zao kwenye kadi ya kutolea fedha kwenye
mashine (ATM).
Mfanyakazi wa Benki hiyo, Tawi la Masdo, Noel Kikoti (30) anadaiwa kuhusika katika wizi huo baada ya kutajwa na mtuhumiwa, Aneth Mwalubanda (29) ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa Sinza Kumekucha.
Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova

alisema Mwalubanda baada ya kukamatwa, alimtaja mfanyakazi huyo akidai anashirikiana naye.
Watuhumiwa wanashikiliwa na polisi na watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kova alisema watu hao walikamatwa katika Benki ya Azania tawi la Mnara wa Mawasiliano barabara ya Sam Nujoma. Inadaiwa walikuwa wakifanya wizi huo kupitia akaunti namba 001001032208270001 mali ya Pamotse Hardware and General Store.
“Mbali na akaunti hiyo watuhumiwa hao kwa pamoja wameshirikiana kuziibia akaunti nyingine tatu za wateja wa akaunti hiyo na huwa wanatumia mbinu ya kuhamisha akaunti iliyolala yaani ‘dormant account’,” alisema Kova. Alisema hutumia mbinu ya kuhamisha akaunti iliyolala ya mtu kisha kubadilisha picha na saini kwa kuondoa picha halali na kuweka ya mtuhumiwa na kadi ya ATM.
via HabariLeo

No comments:
Post a Comment