EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, June 27, 2013

WAKILI WA HENRY KILEO NA JOYCE KIRIA AFUNGUKA.

RE: HENRY JOHN KILEO.


BAADA YA SINTOFAHAMU KUHUSU KILICHOMSIBU HASA HENRY JOHN KILEO, NA BAADA YA MAJIBU YA JESHI LA POLICE KUHUSU JUHUDI ZA JOYCE KIRIA KILEWO KUFAHAMISHWA ALIKO MUMEWE HENRY JOHN KILEWO, NA BAADA YA MASWALI MENGI KWANGU KAMA WAKILI WA KILEWO NA KIRIA, NIMEONA YAFAA NITOE MAELEZO HAYA KWA KIREFU.


 Henry John Kileo alipiwa simu na Maafisa wa Police Makao Makuu mnamo Tarehe 17/6/2013, wakimuarifu kwamba wanataka kufanya mahojiano naye.Hawakusema ni kuhusu nini.mara moja Kilewo akawasiliana nami kama wakili wa familia yao na Joyce Kiria,nami nikawasiliana na maafisa hao kuwaarifu kwamba kwa kuwa nina majukumu kadhaa ya kkimahakama, na kwa kuwa Kilewo yuko nje ya mkoa,basi ninaahidi kama wakili kuhakikisha ninamepeleka binafsi Kilewo Makao Makuu Police mnamo Ijumaa ya tarehe 21/6/2013.

Tarehe 21/6/2013 tuliambatana mimi, Kilewo na John Mnyika (MB) mpaka Police Makao Makuu, ambapo Mnyika alituacha na Kilewo;mahojiano yakaanza.Kwa ujumla walimuhoji Kilewo mambo mbalimbali kuhusiana na tukio la kumwagiwa tindikali kijana aitwaye Mussa Tesha katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga mnamo mwaka 2011.Wakati mahijiano hayo yanafanyika,tayari kulikuwa na Case ya jinai ikiendelea huko Igunga, ambapo washtakiwa Wanne (4) ambao ni makada wa Chadema kutoka maeneo mbalimbali nchini walishtakiwa kama mshtakiwa nambari moja mpaka nne.Walishtakiwa kuhusiana na tukio hilo nililolisema, la Mussa Tesha kumwagiwa Tindikali.Walishtakiwa chini ya vifungu vya sheria ya kanuni ya adhabu, (Penal Code, na si ugaidi).

Baada ya mahojiano na Police yaliyomalizika kwa Kileo kuandikisha statement mpaka mnamo saa 11.30 hivi za jioni ya hiyo Tarehe 21/6/2013, Police walimnyima Kilewo dhamana, na wakampeleka remand iliyoko Central Police Station,akalala huko.
Jumamosi ya mnamo tarehe 22/6/2013, mimi wakili, Joyce Kiria na John Mnyika tulifika Central Police station, ambapo OCS wa hiyo Central Police Station alituarifu kwamba amri alizonazo ni kwamba Kilewo haruhusiwi kuonana na mtu yeyote. Kama wakili nilijadiliana masuala ya kisheria na OCS, ikalazimu kuwasiliana na maafisa wa Police Makao Makuu ambao hatimaye waliniruhusu mimi kama wakili kwa mujibu wa sheria kuonana na mteja wangu.

Tukazungumza na kupeana "moyo", nikahakikisha amekula chakula kilicoletwa na mkewe Joyce Kiria (ambaye muda wote alikuwa akimuangalia mumewe kwa mbali tu,kwani mazungumzo yangu na Kilewo yalifanyika faragha).

Mnamo saa 7.30 hivi tuliondoka sote (wakili, Kiria na Mnyika), na kukubaliana kurudi tena Central Police Station Jumapili ya Tarehe 23/6/2013 kumtembelea tena Kilewo, na pia kufahamu mipango hasa ya jeshi la Police kuhusu Kilewo kwani mpaka tunaondoka si wakili wala mkewe Kilewo aliyefahamishwa rasmi kuhusu mipango hiyo.

Nikiwa Nyumbani nilipokea simu toka kwa Joyce Kiria akiniarifu kwamba amefika Central Police Station jioni ya Jumamosi ya tarehe 22/6/2013 na kuarifiwa tu kwa mkato kwamba Henry John Kilewo "ameondoka".

Ukweli kama mke alikuwa amechanganyikiwa, na jukumu la kwanza lilikuwa kumtuliza kisaikoilojia kwani nilifahamu kina Kilewo walikuwa wamepata mtoto muda si mrefu huko nyuma;kwa hiyo hali ya Joyce ilikuwa delicate sana kiafya na kisaikolojia.
Nikapambana kama wakili kwa kutumia uzoefu na contacts (P.R) ili kupata tarifa ya aliko mteja wangu.

Niliariwa tu "off record" na maafisa wa Police kwamba Kilewo amesafrishwa kwa ndege ya Precision kuelekea Tabora kupitia Mwanza chini ya ulinzi wa maafisa Senior wa Police ili kule Tabora afunguliwe Case.Sikuwa na mawasiliano yeyote na mteja wangu, na hizo taarifa "off record" ndo cha pekee tulichokuwa nacho mimi, Joyce Kiria na uongozi wa Chadema kuhusu nini kimemsibu Henry Kileo.

Niliendelea kupambana kupata taarifa rasmi, na hatimaye Jumapili ya Tarehe 23/6/2013 majira ya saa 6 hivi (noon) ndipo nilipopigiwa simu na mmoja wa maafisa waliomsindikiza Kilewo kuelekea huko Tabora kwa utaratibu ule ule wa "off record", na kuniunganisha na Kilewo, ambapo nilizungumza naye kwa kifupi kumjulia hali na kumuhakikishia kwamba tutapigana kwa uwakili wetu wote kwa ajili yake.

Kwa hiyo mpaka muda huo hatukuwa bado na uhakika wa 100% kwamba Kilewo yuko wapi hasa. Kw wale mawakili wenzangu wanafahamu kwamba huwezi tegemea taarifa za kusikilizishwa mteja kwenye simu ambayo hata si ya kwake.Wala huo si ushahidi wa alipo mtu huyo kisheria.

Lakini ikatubidi ku-"assume" kwamba Kilewo yuko/atapelekwa Tabora kushtakiwa.mimi na Prof Abdallah Safari tukaanza maandalizi ya upesi upesi ya safari kuelekea Tabora kwa gari (kwani ndege kuulekea Tabora ni Jumamosi na Jumatatu tu). Tuliondoka kwa gari ya makao makuu ya Chadema Jumapili ya tarehe 23/6/2013, majira ya saa 11.30 hivi za jioni. Tulisafiri usiku kucha, na tulichukuwa "risk" ambazo kwa kawaida tusingechukuwa, ikiwemo kupita katika mapori maarufu kwa utakaji;kilichotusukuma na kutupa moyo ni kwamba Henry John Kilewo yuko mahali ambapo anatuhitaji sana, na hana tumaini lingine bali sisi mawakili wake.

Tukisafiri usuku kucha na kufika Tabora asubuhi ya Jumatatu tarehe 24/6/2013, majira ya saa 2.30 asubuhi;tumechoka hakuna mfano.Tukabadili mavazi upesi upesi na kuvaa suits zetu na kukimbilia mahakama ya Hakimu Mkazi Tabora, ambapo turiarifiwa kuwa wao hawana taarifa zozote za Kilewo. Tukaelekea Makao Makua ya Police Tabora;jibe likawa ni lile.

Maana yake ni kwamba sisi mawakili wa Kilewo, tuko Tabora ambayo ni kubwa has, na hatujui mteja yuko wapi hasa. Nikafanya juhudi zile zile za "off record", na kufahamishwa kwamba Kilewo alishikiliwa Police Station ya Nzega (masaa matatu toka Tabora), na kwamba yuko njiani kuletwa Tabora.Hatukuwa na uhakika bado, ila ilitulazimu kushikilia hako kataarifa kasiko rasmi, na kuendelea na maandalizi ya case.
Majira ya saa 9 hivi za alasiri ya Tarehe 23/6/2013 Kilewo, akiwa chini ya ulinzi mkali sana wa FFU katika Land Cruisers Mbili za Police waliwasili Mahakama ya Hakimu Mkazi Tabora; hajala tangu jana yake.
Alikuwa yeye na wenzake wanne ambao walikuwa wamefutiwa mashtaka kwa hati ya "Nolle Prosequi" huko Igunga, kisha kukamatwa tena mara moja na kusafirishwa kwa ulinzi mkali sana mpaka Tabora.

Ukweli ni kwamba tulivyoonana na Kilewo si mawakili wala KIlewo mwenyewe aliyejizuia kulengwa na machozi;yeye akimshukuru MUNGU kwamba tumepambana na yote mpaka Tabaora kwa ajili yake kwa kasi vile, nasi kwamba hatimaye tumeonana na mteja wetu.

Tukaingia Mahakamani, Kilewo na wenzake wakasomewa mashtaka mawili; moja chini ya sheria ya kuzuia ugaidi kwamba walimteka kwa nia ya ugaidi Mussa Tesha huko Igunga, Tabora na la pili kwamba walimdhuru kwa kumwagia Tindikali.
Makosa ya Ugaidi hayana dhamana.

Mawakili tulipambana na kutoa hoja za kisheria nne (4) dhidi ya uhalali wa mashtaka yenyewe na utaratibu wa kufungua case husika. Tumeoimba mahakama kufuta mashtaka ya ugaidi, au la iamuru kila mshtakiwa arudishwe kushtakiwa mahali alikokamatwa (mfano Kilewo, Dar es Salaam).

Uamuzi wa Mahakama ni tarehe 8/7/2013.

Kabla ya kuondoka Tabora jana, tulipita kumuaga Henry Kilewo na wenzake katika gereza la Uyui. Wote wako na combat zao za chama chao, na wako imara, hasa baada ya kuona mawakili wako imara.

Cha msingi ni kuomba MUNGU aipe mahakama ujasiri.

Peter Kibatala, Advocate.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate