Haruni Sanchawa na Makongoro Oging'
LILE sakata la madai ya uzinzi kulitikisa Kanisa Katoliki nchini bado ni zito ndani ya Parokia ya Kristu Mfalme Tabata Kigango cha Kimanga, jijini Dar es Salaam, Uwazi lina sehemu ya pili ya mkanda huo.

Uchunguzi wa pili wa Uwazi uliofanywa kwa wiki mbili umefanikiwa
kulinasa jengo la ghorofa analodaiwa kulijenga mwenyekiti wa kamati ya
utendaji ya kanisa hilo, Faustin Mchanuzi kwa ajili ya kumhonga ‘nyumba
ndogo’ yake, Dorosta Kengeli. Ghorofa hilo lipo Tabata- Kinyerezi, Dar.
Awali
ilidaiwa kuwa, fedha za kujengea mjengo huo wa kifahari, mwenyekiti
huyo alizichota kutoka kwenye vyanzo vya mapato vya kanisa hilo.
Timu
ya Uwazi kwa kushirikiana na vyanzo vyake makini, mwishoni mwa wiki
iliyopita ilitia timu nyumbani kwa mwanamke huyo anayedaiwa ni hawara wa
mwenyekiti wa kanisa hilo na kufanikisha kupata picha ya mjengo huo
unaodaiwa kugharimu mamilioni ya shilingi.
Mwanamke huyo alipobanwa
na Uwazi kuhusu kujengewa ghorofa hilo, alisema nyumba hiyo ni yake na
kwa sasa anamtambua Mchanuzi kama baba wa watoto wake na si vinginevyo.
Hata hivyo, katika hali isiyokuwa ya kawaida, wakati wa mazungumzo hayo nje ya mjengo huo, mwanamke huyo alikuja juu na kuwataka waandishi wetu wamsubiri aingie ndani na kurudi kutoa ufafanuzi zaidi lakini cha ajabu alipozama alijifungia moja kwa moja.

Jitihada za mapaparazi wetu
kuonana naye tena ziligonga mwamba baada ya kumtuma mtoto wake wa kiume
kutoa ujumbe kwa waandishi kuwa wanatakiwa kuondoka kwa vile mama huyo
asingetoka tena.
Katika toleo la gazeti hili No. 792 la Mei 28 hadi Juni 3, 2013 ukurasa wa mbele kulikuwa na habari yenye kichwa;

UZINZI WATIKISA KANISA KATOLIKI.
Katika habari hiyo, mwenyekiti huyo alidaiwa kumhonga nyumba ya ghorofa nyumba ndogo yake hiyo. Hata hivyo, mtuhumiwa huyo alidai mwanamke huyo si hawara yake bali alikuwa mke wa pili wa ndoa ya mwaka 1993 lakini waliachana baada ya kujiunga na kanisa hilo lililomtaka amwache mke mmoja. Mke wa kwanza alimuoa 1970.
Alisema alimwongezea fedha za ujenzi wa ghorofa hilo kwa vile wakati wanatalikiana, mwanamke huyo alishamzalia watoto watatu.

Lakini
habari mpya kutoka kwa waumini wa kanisa hilo walihoji kwamba ilikuwaje
mwaka 1970 Mchanuzi alimuoa mkewe wa kwanza kwa ndoa ya kanisani halafu
mwaka 1993 amuoe Dorosta tena kwa ndoa ya kanisani wakati yule wa
kwanza bado yu hai? Hivyo, wanaamini mke wa pili ni nyumba ndogo yake.
Kikristo, mume au mke akishafunga ndoa hakuna talaka wala ndoa nyingine mpaka pale mwenza mmoja atakapoaga dunia.
Mei 20, mwaka huu, waumini wa kanisa hilo walimwandikia barua Polycarp Kardinali Pengo wakimtuhumu mwenyekiti huyo na paroko wake wakamtaka kuingilia kati sakata la kanisa hilo.

VIA GLP
No comments:
Post a Comment