Mwandishi Wetu na Mitandao
IMEVUJA! Kumbe Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Rolihlahla Mandela ‘Mzee Madiba’, alishaandika wosia kwenye karatasi moja tu ambapo aliagiza anavyotaka azikwe katika milima iliyojitenga nyumbani kwa mababu zake katika Kijiji cha Qunu, Eastern Cape huko ‘Sauzi’.
Rais huyo wa zamani na kipenzi cha wengi duniani, mwenye umri wa miaka 94, bado yuko mahututi huku ikielezwa kuwa anapumulia mashine katika Hospitali ya Mediclinic Heart iliyopo Pretoria, Sauzi.
WOSIA AKAVYOZIKWA
Habari zinaeleza kuwa Januari, 1996, wakati akiwa bado rais, Mzee Madiba aliripotiwa kuwa alikuwa ameandika wosia ambao ulijaa maelekezo yote juu ya maziko yake.
Mzee Madiba aliagiza kufanyiwa maziko ya kawaida kabisa karibu na kijijini hapo ambako alikulia kwenye Rasi ya Mashariki.
WAPINGANA NA MATAKWA YA DUNIA NZIMA
Kuhusu hilo, wosia ulidaiwa kupingana na matakwa ya dunia nzima, ambayo ingetaka maziko yake yawe makubwa na ya kihistoria.
KABURI
Aliandika kuwa wakati akifurahia kumbukumbu ya kulitumikia taifa hilo akiwa jijini Pretoria, Mzee Madiba angetaka kuzikwa katika eneo la familia hiyo na kuwekewa jiwe la kawaida kama alama ya lilipo kaburi lake.
HATAKI
Katika tafsiri ya maneno hayo, Mzee Madiba alitaka kaburi lake liwe la kawaida kabisa, lisijengewe kama ilivyokuwa kwa kaburi la Mwalimu Julius Nyerere wa Tanzania na lile la Kamuzu Banda, aliyekuwa Rais wa Malawi.
HATAKI UFAHARI
Magazeti ya South African Mail na Guardian yaliripoti yakimnukuu rafiki wa siku nyingi wa familia akisema: “Hakuwahi (Madiba) kukifanya kifo kuwa jambo kubwa la kufikiriwa, pia hakuwahi kutaka chochote cha ufahari.”
Licha ya ukweli kwamba mauzo ya Kitabu cha Mandela cha Long Walk To Freedom na michoro yenye jina lake, humpatia mamilioni ya fedha, wosia wake uliripotiwa kutosha kwenye karatasi moja tu.
MSHANGAO
Wosia huo ulielezwa kuwashangaza watu wengi duniani kwani waliamini angekuwa na vitu vingi vya kuandika.
Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Afrika Kusini, SABC, swali hilo la sehemu atakayozikwa Mzee Madiba liliiudhi mno familia yake wiki iliyopita.
WANAFAMILIA
Binti mkubwa wa Mandela, Makaziwe Mandela na wanafamilia wengine 15 wameiomba mahakama imwamuru mjukuu wa Mzee Madiba, Mandla Mandela kurejesha miili ya watoto watatu wa familia hiyo kwenye makaburi yao ya awali huko Qunu kwa kuwa alizika sehemu tofauti na eneo hilo.
Mjukuu huyo anaaminika kuizika upya miili hiyo maili 13 kutoka hapo katika Kijiji cha Mvezo ambako anapanga kuanzisha madhabahu ya Mzee Madiba, hoteli na uwanja wa soka.
Familia hiyo ilimpa Mandla muda wa siku kadhaa awe amejibu madai hayo yaliyowasilishwa mahakamani.
Mzee Madiba alijenga makazi yake baada ya kustaafu huko Qunu na alikuwa akiishi hapo hadi alipokimbizwa hospitali mara ya mwisho.
Kiongozi huyo wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi, alihudhuria mazishi ya mtoto wake wa kiume kwenye eneo la familia huko Qunu mwaka 2005 na ilitabiriwa kwa mapana kwamba naye atazikwa hapo.
Ilielezwa kuwa mjukuu wake huyo alihamisha miili ya watoto watatu wa Mzee Madiba na kuipeleka huko Mvezo ambako ni sehemu aliyozaliwa rais huyo wa zamani na mjukuu huyo ana mamlaka kama chifu.
Binti mkubwa wa Mzee Madiba, Makaziwe Mandela na wanafamilia wengine wanataka miili hiyo ya familia kurejeshwa kwenye makaburi yao ya awali huko Qunu.
HALI IKOJE?
Mzee Madiba ambaye atatimiza umri wa miaka 95 Julai 18, mwaka huu, amekuwa hospitalini kwa karibu mwezi mmoja sasa akitibiwa maambukizi kwenye mapafu huku akipumulia mashine.
Bado dunia inaendelea kumuombea usiku na mchana Mzee Madiba apate siha njema na aruhusiwe kutoka hospitalini, maisha yaendelee.

No comments:
Post a Comment