Jaji Mkuu wa Mahakama ya Kikatiba nchini Misri, Adli Mansour
anatarajiwa kuapishwa kama rais wa mpito wa nchi hiyo baada ya jeshi
kumng'oa madarakani rais Mohammed Morsi, ambaye ni kiongozi wa kwanza
kuchaguliwa kidemokrasia nchini humo.
Mkuu wa Jeshi, Generali Abdul Fattah al-Sisi alitoa tangazo hilo kupitia televisheni Jumatano jioni.
Mkuu wa Jeshi, Generali Abdul Fattah al-Sisi alitoa tangazo hilo kupitia televisheni Jumatano jioni.
Generali Sisi alisema kuwa Morsi, ambaye ni rais wa kwanza kuchaguliwa amekosa kutimiza mahitaji ya watu.
Hatua hiyo inakuja baada ya siku nyingi za maandamano dhidi ya rais Morsi wa chama cha Muslim Brotherhood.
Waandamanaji walimtuhumu yeye na chama chake kwa kusukuma ajenda ya
Kiislamu kwa taifa hilo na kukosa kusuluhisha matatizo ya kiuchumi
yanayolikumba taifa hilo.
Chama cha Muslim Brotherhood kimesema kuwa bwana Morsi pamoja na
washauri wake wako chini ya kifungo cha ndani na hawana mawasiliano ya
nje.
Hapo awali, Mkuu wa Majeshi alisema kuwa jaji mkuu wa taifa hilo atachukuwa mamlaka ya rais.
Maelfu ya waandamanaji wanaompinga bwana Morsi mjini Cairo
walisherehekea kwa shangwe na vifijo kufuatia taarifa hiyo ya jeshi
lakini wale wanaomuunga mkono bwana wanasemekana kubaki kimya huku
wakisubiri matukio yatakayofuata.
Rais Obama amesema kuwa ana wasiwasi mkubwa kuhusiana na matukio
yaliyopo nchini Misri huku Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Banki Moon
akitaka kuwe na utulivu.
(Habari: BBC Swahili)
No comments:
Post a Comment